IMEWEKWA JUNI 17, 2013 SAA 5:30 ASUBUHI
MABAO ya Pedro na Roberto Soldado yameiwezesha Hispania kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Uruguay katika mchezo wa Kombe la Mabara jana mjini Recife.
Luiz Suarez aliifungia Uruguay bao la kufutia machozi, lakini mabingwa wa dunia na Ulaya walitawakla mchezo huo mwanzo hadi mwisho na wangeweza kuibuka na ushindi mnene zaidi.
Pedro alifunga dakika ya 20 na Soldado dakika ya 32, wakati Suarez alifunga dakika ya 88.
Kikosi cha Hispania jana kilikuwa: Casillas, Arbeloa, Sergio Ramos, Pique, Jordi Alba, Xavi/Javi Martinez dk77, Busquets, Fabregas/Cazorla dk65, Pedro/Mata dk81, Soldado na Iniesta.
Uruguay: Muslera, Maxi Pereira, Lugano, Godin, Caceres, Rodriguez, Gargano/Lodeiro dk63, Perez/Forlan dk69, Ramirez/Gonzalez dk46, Suarez na Cavani.
Hispania watacheza tena na Tahiti Alhamisi, wakati Uruguay wataivaa Nigeria siku hiyo pia. Nigeria leo watamenyana na mabingwa wa Oceania, Tahiti katika mechi nyingine ya Kundi B mjini Belo Horizonte.
Roberto Soldado akishangilia na wenzake
Luis Suarez akishangilia bao lake
Suarez akipiga mpira wa adhabu
Iker Casillas alishindwa kuokoa mpira wa adhabu wa Suarez
Alvaro Arbeloa akikabiliana na Cristian Rodriguez
Luis Suarez akimtoka Ramos