Mabingwa: Nyota wa U21 ya Hispania wakishangilia na taji lao baada ya kuifumua Italia 4-2
IMEWEKWA JUNI 18, 2013 SAA 3:30 USIKU
KIUNGO Thiago Alcantara amekuwa kivutio katika ushindi wa kikosi cha vijana cha Hispania chini ya miaka 21 wa mabao 4-2 dhidi ya Italia na kutwaa Kombe la Ulaya kwa vijana barani humo, baada ya mchezaji huyo anayetakiwa na Manchester United kufunga mabao matatu mjini Jerusalem.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 wa Barcelona amekuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa na kuhamia Old Trafford.
Alcantara, aliyekuwamo kwenye kikosi cha Hispania kilichoshinda taji hilo miaka miwili iliyopita nchini Denmark, aliifungia timu yake bao la kwanza dakika ya sita, lakini Italia ikasawazisha haraka kupitia kwa Ciro Immobile dakika ya 10.
Thiago akafunga tena dakika ya 31 na 38 kwa penalti, kabla ya Isco kufunga dakika ya 66 kwa penalti pia na Borini akaifungia Italia dakika ya 79 kufanya 4-2.
Kikosi cha Hispania leo kilikuwa; De Gea, Montoya, Bartra, Martinez, Moreno, Koke/Camacho dk86, Illarramendi, Thiago, Tello/Muniain dk70, Morata/Rodrigo dk80 na Isco.
Italy U21; Bardi, Donati, Bianchetti, Caldirola, Regini, Florenzi/Saponara dk58, Rossi, Verratti/Crimi dk76, Insigne, Borini na Immobile/Gabbiadini dk58.
Shujaa wa Hat-trick: Thiago Alcantara amefunga mabao matatu kipindi cha kwanza kuipa ushindi Hispania
Nyota wa Hispania wakishangilia bao la Isco
Alessandro Florenzi wa Italia
Lorenzo Insigne wa Italia (kushoto) akimtoka beki wa Hispania, Martin Montoya
Aberto Moreno wa Hispania akijaribu kumpitia Ciro Immobile wa Italia
Shujaa: Thiago Alcantara (katikati) akishangilia bao lake la tatu na Cristian Tello (mbele) na Alvaro Morata
Kutoka kushoto; Giulio Donati, Matteo Bianchetti na Marco Verratti wakilalamikia penalti
Cristian Tello wa Hispania (kushoto) akikabiliana na Lorenzo Insigne wa Italia
Montoya wa Hispania (kushoto) akienda chini baada ya kupitiwa na Vasco Regini wa Italia