IMEWEKWA JUNI 2, 2013 SAA 1:35 USIKU
KOCHA Sir Alex Ferguson alikuwa jukwaani akishuhudia magwiji wa Old Trafford wakimenyana na magwiji wa Real Madrid katika mchezo wa kirafiki wa hisani.
Bryan Robson aliiongoza timu hiyo ya England mbele ya mashabiki zaidi ya 60,000 ikilala 2-1 kwa Real Madrid.
Sir Alex Ferguson na Sir Bobby Charlton
Picha ya pamoja ya magwiji wa Real Madrid na Manchester United
Jaap Stam akipambana na Ruud van Nistelrooy, ambaye aliichezea kila timu kipindi kimoja
Zinedine Zidane akimtoka Denis Irwin
VIKOSI:
Manchester United: Van der Sar, van der Gouw; Berg, Blackmore, Irwin, Johnsen, Martin, Stam; Fortune, Robson, Scholes, Sharpe; Cole, van Nistelrooy, Yorke.
Real Madrid: Contreras, Sanchez; Cannavaro, Helguera, Hierro, Pavon, Salgado, Sanz; Amavisca, De la Red, Figo, McManaman, Makelele, Zidane; Alfonso, Butragueno, Morientes, van Nistelrooy.
Real Madrid: Contreras, Sanchez; Cannavaro, Helguera, Hierro, Pavon, Salgado, Sanz; Amavisca, De la Red, Figo, McManaman, Makelele, Zidane; Alfonso, Butragueno, Morientes, van Nistelrooy.
Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Fernando Morientes aliifungia bao la kwanza Real na Ruud van Nistelrooy, ambaye aliichezea kila timu kipindi kimoja, akaisawazishia United.
Sekunde kadhaa baada ya Dwight Yorke kugongesha mpira kwenye mwamba wa juu, Ruben de la Red akafunga bao la ushindi zikiwa zimesalia dakika tano.
Edwin van der Sar alikuwa bora alikuwa nyota wa mchezo kwa upande wa United kwa kuokoa michomo kadhaa ya hatari kabla ya kumpisha Raymond van der Gouw kipindi cha pili.
Ruud van Nistelrooy baada ya kuifungia United
Magwiji wa Real Madrid wakimpongeza Fernando Morientes
Dwight Yorke akipiga shuti pembeni ya Francisco Pavon
Claude Makelele akipambana na Paul Scholes
Edwin van der Sar aliokoa sana
Andy Cole alidhibitiwa
Fernando Hierro na Denis Irwin walikuwa Manahodha