IMEWEKWA JUNI 24, 2013 SAA 11:50 JIONI
WASHINDI wa mataji matatu, Bayern Munich wamemtambulisha kocha wao mpya, Pep Guardiola leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari, The Bavarians wakijiandaa kuendelea kutamba katika soka ya nyumbani na Ulaya.
Kocha huyo wa zamani wa Barcelona amesema yuko tayari kukabiliana na changamoto za kufundisha timu iliyofanya vizuri msimu uliopita chini ya Jupp Heynckes, ikishinda mataji ya Ligi Kuu ya nyumbani na makombe mawili, pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
"Lazima nikubali mlinganisho," alisema Guardiola, akiwa katika vazi nadhifu la suti ya vipande vitatu ya rangi ya kijivu akizungumza Kijerumani kwenye Mkutano uliofanyika ukumbi wa mikutano wa klabu, Allianz Arena.
Shinikizo? Pep Guardiola anakuwa kocha wa mabingwa wapya wa Ulaya, Bayern Munich
"Lazima niwe tayari kuishi na hiyo. Nipo chini ya shinikizo, wazi, lakini nafahamu hili na nakubali changamoto hii bila woga na ndiyo maana mimi ni kocha,"alisema.
Guardiola, ambaye aliyeshinda mataji 14 katika miaka minne ya kuwa na Barcelona, usajili wake ni mkubwa Bayern na hasa ikizingatiwa anahamia timu iliyofanya vyema. Alitumia mwaka wake mzima baada ya kuacha kazi Hispania mwaka 2012, kwa kupumzika New York, Marekani.
"Kitu nachofikiria kwa sasa ni zawadi, baraka kuwa hapa na Bayern,"alisema kocha huyo Mspanyola, aliyesaini Mkataba wa miaka mitatu.
Kujiamini: Guardiola akizungumza leo
Waliohudhuria mkutano huo wa kutambulishwa Guardiola bosi mpya Bayern
Wanne mashuhuri: Guardiola aliungana na Matthias Sammer, Karl-Heinz Rummenigge na Uli Hoeness
Aisema sababu ya kwanza iliyomfanya akubali ofa ya kuifundisha Bayern ni wachezaji wa klabu hiyo na historia yake.
Karibu, Pep! Kocha tayari anajisikia nyumbani katikati ya watu
Kiroho safi? Guardiola akiwa na kocha anayeondolewa Bayern, Jupp Heynckes.