IMEWEKWA JUNI 27, 2013 SAA 1:00 ASUBUHI
KLABU ya Barcelona itakuwa na mazungumzo mazito kwa mara ya mwisho na Thiago Alcantara kujaribu kumzuia kiungo huyo wa Hispania asitimkie Manchester United.
KLABU ya Barcelona itakuwa na mazungumzo mazito kwa mara ya mwisho na Thiago Alcantara kujaribu kumzuia kiungo huyo wa Hispania asitimkie Manchester United.
Mabingwa wa Ligi Kuu ya England wamekubaliana na mchezaji huyo kumlipa mshahara wa Pauni Milioni 5.5 kwa mwaka kupitia kwa baba yake Thiago, aliyewahi kutwaa Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha Brazil, Mazinho, na wana uhakika wa kumalizia dili kwa kuilipa Pauni Milioni 17 klabu yake ya uhamisho.
Barca bado ina matumaini ya kumbakiza kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa kumuahidi atakuwa kiongozi klabu hiyo kwa miaka ijayo, lakini anabakia kuwa asiyeshawishika baada ya kusotea namba kwenye kikosi cha kwanza.
Anabaki, habaki: Thiago Alcantara, akiwa na taji la Ulaya la U21, tayari amekubaliana na Manchester United
Thiago amekwenda mapumzikoni, akimuacha baba yake na wawakilishi wake wazungumze na mabingwa hao wa Hispania, ambao wanatarajiwa kuiambia Barcelona kwamba wanataka kutoka Nou Camp kuhamia Old Trafford.
United imefanya jitihada kubwa kuhakikisha inampata mchezaji huyo, ikiamini Manchester City na Bayern Munich wanaweza kutoa ofa.
Inafahamika hawana mpango na mshambuliaji wa Napoli, Edinson Cavani lakini wanaendelea kufuatilia sakata la Mkataba wa Cristiano Ronaldo Real Madrid.
Nyota huyo wa zamani wa United, ameahidiwa Pauni Milioni 12 kwa mwaka ili abaki Bernabeu, lakini anataka Milioni 5 zaidi na hajafirahishwa na maneno ya karibuni ya Rais wa Real, Florentino Perez kwamba kila kitu kina kiwango chake.
Shujaa anarudi? United inaangalia uwezekano wa kumrejesha Cristiano Ronaldo
Kocha mpya: David Moyes anataka kujenga kikosi imara kabla ya kuanza kazi rasmi United