IMEWEKWA JUNI 8, 2013 SAA 6:38 MCHANA
MSHAMBULIAJI Mario Balotelli alipiga ngumi ukuta baada ya kulimwa kadi nyekundu Italia ikitoka sare ya 0-0 na Jamhuri ya Czech mjini Prague.
Mshambuliaji huyo wa AC Milan alitolewa nje zikiwa zimesalia dakika 20 lakini akawawakia refe na benchi la ufundi la Italia na viongozi, kabla ya kumalizia hasira zake kwa kupiga ngumi ukuta wakati anatoka nje.
VIDEO Mario Balotelli akilimwa kadi nyekundu Prague
Hasira: Mario Balotelli akimalizia hasira zake kwa kupiga ngumi ukutani
Nenda nje: Mario Balotelli akionyeshwa kadi nyekundu
Si haki: Balotelli hakuona kama alistahili kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Theodor Gebre Selassie
Balotelli anaondoka huku Gabre Selassie akilalamika chini
Faulo iliyomponza alimchezea beki wa kulia wa Czech, Theodore Gabre Selassie, baada ya Balotelli kumpa mkono wa usoni beki huyo wakati wa kugombea mpira.
Sare hiyo inaiweka kileleni mwa Kundi B Italia katika mbio za kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia, kwa pointi nne zaidi ya Bulgaria walio nafasi ya pili.
Czech inabaki nafasi ya tatu, nyuma ya Bulgaria.