IMEWEKWA JUNI 17, 2013 SAA 5:50 ASUBUHI
MSHAMBULIAJI Mario Balotelli alifunga bao la ushindi kwa Italia, baada ya Andrea Pirlo kutangulia kufunga bao la kuongoza kwa mpira wa adhabu akiichezea nchi yake mechi ya 100 katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mabara.
Balotelli alipokea nzuri ya Emanuele Giaccherini zikiwa zimesalia dakika 12 na akapasua katikati ya mabeki wawili kabla ya kufunga kwenye Uwanja wa Maracana.
Mshambuliaji wa Manchester United, Javier 'Chicharito' Hernandez alifunga kwa penalti dakika ya 34 kuipa Mexico bao la kusawazisha baada ya Andrea Barzagli kumuangusha kiungo wa zamani wa Tottenham, Giovani Dos Santos kwenye boksi.
Hernandez anaelekea kuipiku rekodi ya mabao mengi Mexico, 42 yaliyofungwa na gwiji wa zamani wa nchi hiyo, Jared Borgetti.
Mchezaji bora wa mechi alikuwa Pirlo aliyefunga bao la kwanza dakika ya 27 akimtungua kwa mpira wa adhabu kipa wa Mexico, Jose de Jesus Corona.
Kikosi cha Mexico kilikuwa: Corona, Rodriguez, Salcido, Flores, Moreno, Torrado, Aquino/Mier dk53, Zavala/Jimenez dk85, Guardado, Giovani na Hernandez.
Italia: Buffon, Chiellini, De Sciglio, Abate, Barzagli, Marchisio/Cerci 68, De Rossi, Montolivo, Pirlo, Giaccherini/Aquilani dk88 na Balotelli/Gilardino dk85.
Shujaa: Mario Balotelli akishangilia na Daniele De Rossi a
Balotelli
Mpenzi wa Balotelli, Fanny Neguesha akifurahia mechi kwa kupiga picha
Javier 'Chicharito' Hernandez aliifungia kwa penalti Mexico