IMEWEKWA JUNI 2, 2013 SAA 1:10 ASUBUHI
BEKI Eric Abidal jana alihitimisha miaka yake sita Barcelona na kufanyiwa tafrija nzuri ya kuagwa ndani ya Uwanja wa Nou Camp.
Beki huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 33, ambaye alirejea uwanjani baada ya kupona matatizo ya ini, alipewa jezi ya fremu ya Barca iliyoandikwa 'Merci Abi' na akanyanyuliwa juu na wachezaji wenzake.
Cesc Fabregas, anayetakiwa na Manchester United, Manchester City na Arsenal, na David Villa, anayetakiwa na The Gunners na Tottenham, wanaweza kuwa walicheza mechi yao ya mwisho katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Malaga.
Abidal aliingia uwanjani akitokea benchi dakika ya 75 kuwaaga mashabiki baada ya kutangaza hatasaini tena msimu mwingine mapema wiki hii huku akibubujikwa na machozi.
Eric Abidal akiwa amenyanyuliwa juu na wachezaji wenzake Barcelona
Abidal akiwa na fremu ya jezi aliyopewa
Abidal alisajiliwa kama mchezaji huru kutoka Lyon mwaka 2007 na amecheza karibu mechi 200. Katika miaka yake sita ameshinda mataji manne ya La Liga, mawili ya Ligi ya Mabingwa, mawili Kombe la Mfalme, matatu ya Super Cup ya Hispania na mawili ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA.
Pia aliingizwa kwenye timu ya UEFA ya mwaka 2007 na akashinda tuzo ya beki bora La Liga mwaka 2011.
Cesc Fabregas alifunga bao zuri jana ambalo linaweza kuwa bao lake la mwisho
Mchezaji anayetakiwa na Spurs na Arsenal, David Villa pia alifunga
Abidal akiwa na mpwa wake, Gerard, ambaye alimsaidia wakati wa tiba
Kimataifa alikuwemo kwenye kikosi cha Ufaransa kilichoshika nafasi ya pili katika Kombe la Dunia mwaka 2006 na amecheza jumla ya mechi 61 katika timu hiyo. Pia ameshinda mataji matatu ya Ligue 1 akiwa na Lyon.
Katika Mkutano na Waandishi wa Habari mapema wiki hii alisema: "Ningependa kubaki, lakini lazima nikubaliane na uamuzi wa klabu (kutoniongezea mkataba).
"Lengo langu ni kuendelea kucheza na sijabadilisha mawazo, suala ni afya. Ni siku ngumu sana kwangu,".
Eric Abidal alimwaga machozi alipokuwa anatangaza kuondoka kwake
"Nimecheza hapa kwa miaka sita, na umekuwa uzoefu mkubwa katika maisha yangu. na nilikuwa nina malengo mawili: kupambana mabinti zangu wakue na kucheza tena.
"Nataka kuwashukuru mashabiki wote wa klabu ambao walinisapoti.
"Timu ni familia yangu ya pili. Tumepitia mengi pamoja na nitakumbuka hii daima. NakwendaI, nitahakikisha narudi,"alisema.
Fabregas na Villa wote wanaandamwa na tetesi za kuondoka kwenda kucheza Ligi Kuu England na kiungo wa zamani wa Arsenal, anatarajiwa kuwa na mazungumzo na kocha Tito Vilanova wiki ijayo.
Aliingia dakika ya 75