// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC WAREJEA LEO DAR NA KUFIKIA KATIKA BONGE LA HOTELI 'FULL KIYOYOZI' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC WAREJEA LEO DAR NA KUFIKIA KATIKA BONGE LA HOTELI 'FULL KIYOYOZI' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, May 17, 2013

    YANGA SC WAREJEA LEO DAR NA KUFIKIA KATIKA BONGE LA HOTELI 'FULL KIYOYOZI'

    Baadhi ya wachezaji wa Yanga, Haruna Niyonzima na Godfrey Taita kushoto. Vijana wanarejea leo.

    Na Mwandishi Wetu, IMEWEKWA MEI 16, 2013 SAA 12:10 ASUBUHI
    KIKOSI cha mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kinatarajiwa kurejea leo dar es Salaam, baada ya kambi wiki moja kisiwani Pemba, kujiandaa na mchezo wa kesho wa kufunga pazia la ligi hiyo, dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    BIN ZUBEIRY inafahamu Yanga itawasili leo Dar es Salaam na kufikia katika hoteli moja ya nyota tano ambako italala na kuamkia Taifa kesho. 
    Mapema jana, kocha Mkuu wa Yanga SC, Ernie Brandts alisema anaamini kikosi chake ni bora na ana kila sababu ya kuwafunga wapinzani wake wa jadi, Simba SC kesho.
    Akizungumza akiwa Pemba, ambako timu yake imeweka kambi tangu Ijumaa ikijifua vikali kwa ajili ya mchezo huo, Brandts alisema kwamba matumaini ya ushindi Jumamosi ni makubwa kutokana na ubora wa kikosi chake.
    “Nina timu bora, wachezaji bora, uwezo wa wachezaji wangu ni wa hali ya juu, mshikamano na umoja katika kikosi ni wa hali ya juu, morali na mtazamo wa kila mchezaji ni kuhakikisha tunashinda mchezo huo, kwa hiyo nina kila sababu ya kujivunia kikosi changu kuibuka na ushindi,” alisema Brandts.
    Akiwazungumzia wapinzani wake, beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi, alisema Simba wana timu nzuri, lakini hiyo haimpi presha kwani kikosi cha Yanga kimekamilika kila idara.
    “Nina timu bora. Nia, uwezo na sababu ya kushinda mchezo huo tunayo, hivyo wana Yanga wakae mkao wa kushangilia ushindi na ubingwa siku ya Jumamosi,”alisema.
    Kwa upande wake, Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kikosi chao kipo katika hali nzuri, wachezaji wana morali ya hali ya juu lengo lao ni kuhakikisha wanashinda mchezo wa Jumamosi na kuwapa furaha wana Yanga.
    Kuelekea mchezo huo, Yanga tayari imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu kutokana na pointi zake 57, ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
    Azam FC imejihakikishia nafasi ya pili kwa pointi zake 52 na inaweza kumaliza ligi na pointi 55 ikishinda mechi yake ya mwisho dhidi ya JKT Oljoro keshokutwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha na Simba waliokuwa mabingwa watetezi, watakuwa wa tatu kwa matokeo yoyote keshokutwa.
    Kikosi cha Yanga kilichoweka kambi Samail Hotel, mkabala na beki ya PBZ, kimekuwa kikifanya mazoezi kwenye wa Uwanja wa nyasi bandia wa Gombani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: YANGA SC WAREJEA LEO DAR NA KUFIKIA KATIKA BONGE LA HOTELI 'FULL KIYOYOZI' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top