// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC WAPANGWA KUNDI C LAINI KAGAME, SIMBA KUNDI A LA HATARI TUPU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC WAPANGWA KUNDI C LAINI KAGAME, SIMBA KUNDI A LA HATARI TUPU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Tuesday, May 21, 2013

        YANGA SC WAPANGWA KUNDI C LAINI KAGAME, SIMBA KUNDI A LA HATARI TUPU

        Mabingwa watetezi; Yanga SC wamepangwa Kundi C

        Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA MEI 21, 2013
        SAA 4:00 USIKU
        BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) limewapanga katika Kundi C, mabingwa watetezi, Yanga SC katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati, Kombe la Kagame leo katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Juni 18 hadi Julai 2, mwaka huu mjini Khartoum, Sudan.
        Katika kundi hilo, mabingwa hao mara mbili mfululizo wa taji hilo wamepangwa na Ports ya Djibouti, Express ya Uganda na  Vital 'O'  ya Burundi, wakati wapinzani wao wa jadi, Simba SC wamepangwa kundi A pamoja na wenyeji El-Mereikh, Elman  ya Somalia na APR ya Rwanda
        Mabingwa wa Kenya, Tusker wamepangwa Kundi B pamoja na wenyeji wengine, Al-Hilal, Al Ahly Shandy ya Sudan, Falcons ya Zanzibar na Al-Nasir Juba ya Sudan Kusini.
        Yanga itaanza kampeni zake Juni 20 kwa kumenyana na Express na Simba SC itashuka dimbani Juni 21 kufungua dimba na El-Mereikh, mechi zote zikichezwa Elfashar.
        Katibu wa CECAFA, Nicholas Musonye amesema zawadi za washindi zimeongezeka kutoka dola za Kimarekani 60,000 anazotoa Rais wa Rwanda, Paul Kagame hadi dola 80,000 baada ya Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji kuongeza dola 20,000.
        Lakini Musonye amesema wanataka zawadi za washindi ziwe jumla dola 100,000 hivyo wanatafuta fedha za kuongezea. 
        Wawakilishi; Simba SC wapo Kundi A la kifo


        KUNDI A: El-Merrekh -(Sudan), APR (Rwanda), 
        Simba SC (Tanzania), Elman (Somalia) - EL FASHER
        KUNDI B: Al-Hillal (Sudan), Tusker (Kenya), Al Nasri (Sudan Kusini), Falcon (Zanzibar),  Al Shandy (Sudan) - KADUGLI
        KUNDI C: Yanga SC (Tanzania), Express (Uganda), Ports (Djibout), Vitaloo (Burundi) - EL FASHIR

        RATIBA KOMBE LA KAGAME KUANZIA JUNI 18 HADI JULAI 2, 2013 (EL-FASHIR NA KADUGLI - SUDAN)
        TAREHETIMUTIMUKUNDI/MUDAUWANJA
        18.06.2013.TUSKER SUPER FALCON B - SAA 8:00 MCHANAKADUGLI
        AL HILLAL AL NASRI B -SAA 10:00 JIONIKADUGLI
        19.06.2013.VITALOOPORTS  C - SAA 10:00 JIONIEL-FASHER
        20.06.2013.YANGA SC EXPRESS C - SAA 8:00 MCHANAEL-FASHER
        20.06.2013.ELMAN FC APR FC A - SAA 10:00 JIONIEL-FASHER
        20.06.2013.SUPER FALCON AL NASRI B -SAA 8:00 MCHANAKADUGLI
        20.06.2013.TUSKER AL-SHANDY B -SAA 10:00 JIONIKADUGLI
        21.06.2013.EL MERREIKH SIMBA SC A -SAA 10:00 JIONIKADUGLI
        22.06.2013.EXPRESS FC VITALOO C - SAA 8:00 MCHANAEL-FASHER
        PORTS YANGA SC C -SAA 10:00 JIONIEL FASHER
        22.06.2013.AL NASRITUSKER B - SAA 8:00 MCHANAKADUGLI
        AL SHANDY AL HILAL B -SAA 10:00 JIONIKADUGLI
        23.06.2013APR SIMBA SC A - SAA 8:00 MCHANAEL-FASHER
        EL MERREIKH  ELAM FC A -SAA 10:00 JIONI
        EL-FASHER
        24.06.2013AL NASRI AL SHANDY B -SAA 8:00 MCHANAKADUGLI
        SUPER FALCON AL HILLAL B -SAA 10:00 JIONIKADUGLI
        24.06.2013. PORTSEXPRESS FC C -SAA 10:00 JIONIEL-FASHER
        25.06.2013.VITALOO YANGA SC C -SAA 10:00 JIONIEL-FASHER
        26.06.2013.AL SHANDY SUPER FALCON B -SAA 8:00 MCHANAKADUGLI
        AL HILLAL TUSKER B -SAA 10:00 JIONIKADUGLI
        26.06.2012.SIMBA SC ELMAN FC A -SAA 8:00 MCHANAEL-FASHER
        APR FC EL MERREIK A -SAA 10:00 JIONIEL-FASHER
        27.06.2013.MAPUMZIKOMAPUMZIKOMAPUMZIKO
          MAPUMZIKO
        28.06.2013.(23) B2 VS C2(24) B1 VS BEST QUTATANGAZWAKADUGLI
        28.06.2013.(25) C1 VS A2(26) A1 VS B3UTATANGAZWAEL-FASHER
        30.06.2013.WNR 23 VS WNR 25WIN 24 VS WIN 26UTATANGAZWA
        01.07.2013.MAPUMZIKOMAPUMZIKOMAPUMZIKOMAPUMZIKO
        02.07.2013.ILIYOFUNGWAILIYOFUNGWAMSINDI WA TATUEL-FASHER
         ALIYESHINDA 27 ALIYESHINDA 28  FAINALI EL-FASHER
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments
        Item Reviewed: YANGA SC WAPANGWA KUNDI C LAINI KAGAME, SIMBA KUNDI A LA HATARI TUPU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry