Shindano... |
Na Prince Akbar, IMEWEKWA MEI 28, 2013 SAA 1:50 MCHANA
WAKATI timu ya Ghana jana imeng’arfa katika Nusu Fainali ya kwanza ya shindano la GUINNESS® FOOTBALL CHALLEGE na kujishindia fedha lukuki, Tanzania nayo haiajtoka kappa kabisa, kwani imeambulia kifuta jasho.
Wawakilishi wa Tanzania kwenywe shindano hilo, Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad kutoka Dar es Salaam wamevuna dola za Kimarekani, 5,500, walizojipatia katika hatua za kitaifa.
Wawakilishi wa Ghana, Jonathan Nabb na Desmond Odaano walionyesha umahiri wao walipowashinda wapinzani wao na kujinyakulia kiasi cha dola 12,000.
Jonathan na Desmond walizawadiwa pia dola 4,000 baada ya kuonyesha mchezo mzuri katika mizunguko miwili ya mwanzo ya mchezo, kwa kupatia maswali yote na sasa wamefanikiwa kujihakikishia nafasi katika fainali ya Pan-African na hata kuwa washindi wa mashindano hayo.
Wataungana na Francis Ngigi na Kepha Kimani kutoka Nairobi waliokuwa washindi wa pili.
Wenzao kutoka Kenya Kenneth Kumau na Wills Ogutu hawakufanikiwa kufuzu, hivyo Francis na Kepha ndio watakaowakilisha Afrika Mashariki.
Sasa kazi itakuwa kwa timu mbili za Kenya katika nusu fainalli ijayo watakapokuwa wakiiwakilisha Afrika Mashariki. Mkurugenzi wa GUINNESS alisema; “Sote Tanzania tunawapongeza Daniel na Mwalimu-japokuwa hawakufanikiwa kufuzu fainali lakini wamejishindia kiasi kikubwa cha pesa. Kila timu ilijitahidi kufikia nusu fainali na hongera zao,”alisema.