Didier Kavumbangu kulia na Haruna Niyonzima kushoto wakimdhibiti Mrisho Ngassa katikati |
Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA MEI 19, 2013 SAA 4:50 ASUBUHI
USHINDI wa mabao 2-0 kwa Yanga SC jana dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC ndio mnono zaidi kwao dhidi ya mahasimu wao hao, ndani ya miaka 13 katika Ligi Kuu na miaka 10 kwa ujumla.
Yanga SC jana iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba SC, yaliyotiwa kimiani na Didier Kavumbangu na Hamisi Kiiza moja kila kipindi.
Kabla ya hapo, mara ya mwisho katika Ligi Kuu Yanga kushinda kwa tofauti ya mabao mawili dhidi ya Simba SC, ilikuwa ni Agosti 5, mwaka 2000, wakati mabao ya Iddi Moshi Shaaban yalipoipa timu hiyo ushindi wa 2-0.
Baada ya hapo, Yanga iliuja kupata ushindi mzuri zaidi dhidi ya Simba SC Aprili 20, mwaka 2003 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza 3-0 katika mchezo wa kirafiki uliondaliwa na Dika Sharp, mabao yakifungwa na Kudra Omary dakika ya 30, Heri Morris dakika ya 32 na Salum Athumani dakika ya 47.
Tofauti na hapo, Yanga imekuwa ikishinda 1-0 na 2-1 dhidi ya watani wao hao kwa kipindi chote hicho na zaidi ni wao ndiyo wamekuwa wakitoka vichwa chini mara nyingi baada ya mechi za watani.
Je, 2-0 za jana ni mwanzo wa zama mpya za ubabe wa Yanga kwa Simba?
Mchezaji bora wa mechi ya jana, Athumani Iddi 'Chuji' akimiliki mpira ya Athumani Iddi 'Chuji' |
REKODI YA SIMBA NA YANGA LIGI KUU TANGU 2000:
AGOSTI 5, 2000
Yanga v Simba,
2-0, Uhuru (Dar)
MFUNGAJI: Iddi Moshi 37 na 47.
(Alifunga mabao hayo, akitoka kwenye fungate ya ndoa yake)
SEPTEMBA 1, 2001
Simba v Yanga
1-0, Uhuru (Dar)
MFUNGAJI: Joseph Kaniki dk. 76
SEPTEMBA 30, 2001
Simba v Yanga
1-1, Kirumba (Mwanza)
WAFUNGAJI:
Simba: Joseph Kaniki dk. 65,
Yanga: Sekilojo Chambua dk. 86
AGOSTI 18, 2002
Simba v Yanga
1-1, Uhuru, (Dar)
WAFUNGAJI:
Simba: Madaraka Selemani 65
Yanga: Sekilojo Chambua (penalti). dk. 89
NOVEMBA 10, 2002
Simba v Yanga
0-0, Uhuru (Dar)
SEPTEMBA 28, 2003
Simba v Yanga
2-2, Uhuru (Dar)
WAFUNGAJI:
Simba: Emmanuel Gabriel dk. 27 na 36
Yanga: Kudra Omary dk. 42, Heri Morris dk. 55
NOVEMBA 2, 2003
Simba v Yanga
0-0, Uhuru (Dar)
AGOSTI 7, 2004
Simba v Yanga
2-1, Uhuru (Dar)
WAFUNGAJI:
Simba: Shaaban Kisiga dk. 64, Ulimboka Mwakingwe dk. 76
Yanga: Pitchou Kongo dk. 48
SEPTEMBA 18, 2004
Simba v Yanga
1-0, Uhuru (Dar)
MFUNGAJI: Athumani Machuppa dk. 82
APRILI 17, 2005
Simba v Yanga
2-1, Jamhuri (Moro)
WAFUNGAJI:
Simba: Nurdin Msiga dk. 44, Athumani Machupa dk. 64,
Yanga: Aaron Nyanda dk. 39
AGOSTI 21, 2005
Simba v Yanga
2-0, S.A. Abeid (Arusha)
MFUNGAJI: Nico Nyagawa dk. 22 na 56
MACHI 26, 2006
Simba v Yanga.
0-0, Uhuru (Dar)
OKTOBA 29, 2006
Simba v Yanga
0-0, Uhuru, (Dar)
JULAI 8, 2007
Simba v Yanga
1-1, Jamhuri (Moro)
WAFUNGAJI:
Simba: Moses Odhiambo (penalti dk. 2)
Yanga: Said Maulid (dk. 55).
(Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya sare hiyo 1-1 dakika 120).
OKTOBA 24, 2007:
Simba Vs Yanga
1-0, Jamhuri (Moro)
Mfungaji: Ulimboka Mwakingwe
APRILI 27, 2008:
Simba Vs Yanga
0-0, Uhuru (Dar)
OKT 26, 2008
Yanga Vs Simba
1-0, Taifa (Dar)
MFUNGAJI: Ben Mwalala dk15.
APRILI 19, 2009
Simba Vs Yanga
2-2, Taifa (Dar)
WAFUNGAJI:
SIMBA: Ramadhan Chombo dk 23, Haruna Moshi dk 62
YANGA: Ben Mwalala dk48, Jerry Tegete dk90
OKTOBA 31, 2009
Simba Vs Yanga
1-0, Taifa (Dar)
MFUNGAJI: Mussa Hassan Mgosi dk 26
APRILI 18, 2010
Simba Vs Yanga
4-3, Taifa (Dar)
WAFUNGAJI:
SIMBA: Uhuru Suleiman dk 3, Mussa Mgosi dk 53 na 74, Hillary Echesa dk 90+
YANGA: Athumani Iddi dk 30, Jerry Tegete dk 69 na 89
OKTOBA 16, 2010:
Yanga Vs Simba
1-0, Kirumba, Mwanza
MFUNGAJI: Jerry Tegete dk 70
MACHI 5, 2011
Simba Vs Yanga
1-1, Taifa (Dar)
WAFUNGAJI:
YANGA: Stefano Mwasyika (penalti) dk 59.
SIMBA: Mussa Mgosi dk 73.
(Refa Orden Mbaga alizua tafrani uwanjani, kwanza kwa kulikataa bao la kusawazisha la Simba, kisha akalikubali baada ya kujadiliana na msaidia wake namba moja)
OKTOBA 29, 2011
Yanga Vs Simba
1-0, Taifa (Dar)
MFUNGAJI: Davies Mwape dakika ya 75
MEI 6, 2012
Simba Vs Yanga SC
5-0, Taifa (Dar),
WAFUNGAJI:
Emmanuel Okwi (dk 2 na 62), Felix Sunzu (penalti 56), Juma Kaseja (penalti dk 67) na Patrick Mafisango (penalti dk 72)
OKTOBA 3, 2013
Simba Vs Yanga SC
1-1, Taifa (Dar)
WAFUNGAJI:
Simba SC: Amri Kiemba dk3
Yanga SC: Said Bahanuzi dk65
(Ligi Kuu)
MEI 18, 2013
Yanga Vs Simba SC
2-0, Taifa (Dar)
WAFUNGAJI: Didier Kavumbangu dk 5 na Hamisi Kiiza dk 62.
Mashabiki wa Yanga jana |