IMEWEKWA MEI 16, 2013 SAA 9:00 ALASIRI
MSHAMBULIAJI Fernando Torres alionekana kama amekwisha tangu aondoke Liverpool na kutua Chelsea miaka miwili na nusu iliyopita kwa dau la Pauni Milioni 50.
Lakini, baada ya Chelsea kutwaa taji lao la pili Ulaya kwa kuifunga Benfica usiku wa jana Uwanja wa Amsterdam, Torres sasa ni mshindi wa mataji manne makubwa Ulaya, kwa klabu na timu yake ya taifa.
Bayern Munich au Borussia Dortmund hawawezi kuchukua taji la Ligi ya Mabingwa la The Blues hadi Jumamosi ijayo, na pamoja na hayo ana mataji ya Euro na Kombe la Dunia, na Europa League linakamilisha seti ya mataji makubwa kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid.
Mwali wa fedha: Fernando Torres akiwa na taji la Europa League Amsterdam jana
Na lingine tena: Torres akikimbia na Kombe la Ligi ya Mabingwa kwenye Uwanja wa Allianz Arena msimu uliopita
Na Torres, ambaye msimu huu amemudu kufunga zaidi ya mabao 20 kwa mara ya kwanza ndani ya miaka mitatu, ametoa mchango mkubwa kuisaidia klabu na nchi yake kufikia mafanikio hayo.
Kwa kufunga bao la ushindi katika Euro 2008 dhidi ya Ujerumani kwenye fainali, Torres aitwaa kiati cha dhahabu katika fainali za Euro 2012 baada ya kuifunga Hispania katika fainali dhidi ya Italia ya Mario Balotelli.
Licha ya kuanza katika mechi mbili tu, Torres alimudu kufunga mabao matatu. Wachezaji sita walifunga mabao matatu pia ambao ni Mario Gomez (Ujerumani), Alan Dzagoev (Urusi), Mario Mandzukic (Croatia), Cristiano Ronaldo (Ureno) na Balotelli.
Lakini pasi ya mshambuliaji huyo wa Hispania dakika ya 88 kwa Juan Mata kufunga bao la nne la Hispania kwenye fainali lilimfanya Torres awabwage wapinzani wake.
Nchini kwake! Torres akiwa ameinua Kombe la Euro mwaka 2008
Raha iliyoje: Torres akiwa na Kombe la DuniaAfrika Kusini
Furaha: Torres na wachezaji wenzake wa Hispania wakiwa na Kombe la Euro mwska 2012
Mtu babu kubwa: Torres alifanikiwa kutwaa kiatu cha dhahabu licha ya kucheza mechi mbili tu katika kikosi cha Vicente Del Bosque