// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC YATAKA KUSAJILI MKALI KULIKO OKWI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC YATAKA KUSAJILI MKALI KULIKO OKWI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, May 29, 2013

    SIMBA SC YATAKA KUSAJILI MKALI KULIKO OKWI

    Kifaa cha ukweli; Moses Oloya yuko mbioni kutua Simba SC

    Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA MEI 29, 2013 SAA 1:15 ASUBUHI
    KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Moses Oloya (20) yupo katika mazungumzo na na klabu ya Simba SC, ambayo yanaendelea vizuri.
    Tayari mshambuliaji huyo wa Saigon Xuan Thanh ya Vietnam amerejea Kampala, Uganda kujiunga na timu yake ya taifa, kwa ajili ya mechi ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia.
    Kiongozi wa Simba SC yupo Uganda tayari na anaendelea na mazungumzo na kiungo huyo, ambaye aling’ara katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwishoni mwa mwaka jana na kuiwezesha Uganda kutwaa Kombe.
    Kiongozi huyo aliyefanikisha usajili wa Mganda mwingine, beki Samuel Ssenkoom wa URA, amefikia sehemu nzuri katika mazungumzo na mchezaji huyo mwenye nguvu, kasi na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira. 
    Bila shaka, kama mazungumzo yataendelea vizuri, ndani ya siku mbili Oloya atasaini Simba SC.
    Na ikimpata mchezaji huyo aliyezaliwa Oktoba 22, mwaka 1992, akitokea KCC ya kwao, aliyoichezea tangu 2009 hadi 2010, Simba itakuwa imelamba dume.
    Oloya ni mchezaji mzuri kuliko Emmanuel Okwi ambaye Simba SC imemuuza Etoile du Sahel ya Tunisia na Desemba mwaka jana, Yanga SC na Azam zote zilijaribu kutaka kumsajili bila mafanikio.
    Mwishowe Azam ikaona bora kumsajili Brian Umony, wakati Yanga ilibanwa na nafasi ya idadi ya wachezaji wa kigeni, lakini ikamuweka kwenye orodha ya wachezaji inayoweza kuwasajili kwa ajili ya msimu ujao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIMBA SC YATAKA KUSAJILI MKALI KULIKO OKWI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top