// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC WANAKULA KIPUPWE HOLIDAY INN HOTEL MIDA HII - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC WANAKULA KIPUPWE HOLIDAY INN HOTEL MIDA HII - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, May 17, 2013

    SIMBA SC WANAKULA KIPUPWE HOLIDAY INN HOTEL MIDA HII

    Wachezaji wa Simba SC wanakula kiyoyozi Holiday Inn mida hii

    Na Prince Akbar, IMEWEKWA MEI 17, 2013 SAA 3:41 USIKU
    KIKOSI cha waliokuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kimeweka kambi katika hoteli ya Holiday Inn, katikati ya Jiji la Dar es Salaam leo kikitokea visiwani Zanzibar kilipokuwa kwa wiki nzima kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga SC kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Wachezaji wapo vizuri katika hoteli hiyo, ambayo zamani ilikuwa inajulikana kama Mawenzi kuelekea mchezo wa kesho. 
    Wachezaji hao, wamewaahidi Friends of Simba kwamba kesho wataifunga na hakuna shaka juu ya hilo.
    “Tumezungumza na vijana, tumewatembelea hapa kambini, wako vizuri na wametuhakikishia Jumamosi wanamnyoa Yanga akashangilie ubingwa chumbani kwake, si mbele yao,”alisema Mwenyekiti wa Friends of Simba, alipozungumza na BIN ZUBEIRY jana usiku.
    Hans Poppe alisema kuhusu wamewaandalia nini iwapo watashinda mechi hiyo, watawaambia wakifika Dar es Salaam. “Bahasha ya ahadi ya bakhshishi yao tutawafungulia watakapotua Dar es Salaam kutoka Zanzibar (kesho) saa chache kabla ya kwenda uwanjani,”alisema Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ). 
    Simba SC imeweka kambi maeneo ya Mbweni, Zanzibar ikifanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Mao Dze Tung katikati ya mjini huo wa kitalii. 
    Mchezo wa kesho unatarajiwa kuchezeshwa na refa Martin Saanya kutoka Morogoro, akisaidiwa na Samuel Mpenzu wa Arusha na Jesse Erasmo kutoka Morogoro, wakati refa akiba atakuwa ni Hashim Abdallah wa Dar es Salaam.
    Kamisaa wa mechi hiyo atakuwa Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya wakati mtathmini wa waamuzi atakuwa ni Leslie Liunda wa Dar es Salaam.
    Mashabiki watakaotaka kwenda kushuhudia mpambano huo wa mahasimu wa jadi katika soka ya Tanzania, watalazimika kulipa Sh. 5,000, hicho kikiwa kiingilio cha chini zaidi katika sehemu ya viti vya Rangi ya Bluu. 
    Aidha, katika mchezo huo utakaoanza saa 10:00 jioni, viingilio vingine ‘nafuu kidogo’ vitakuwa ni Sh 7,000 kwa viti ya Rangi ya Kijani na Sh. 10,000 kwa viti vya Rangi ya Chungwa.
    Upande wa ‘wakubwa’, viingilio vitakuwa ni Sh. 15,000 kwa VIP C, Sh. 20,000 kwa VIP B na Sh. 30,000 kwa VIP A na tiketi zitaanza kuuzwa kesho.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIMBA SC WANAKULA KIPUPWE HOLIDAY INN HOTEL MIDA HII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top