IMEWEKWA MEI 17, 2013 SAA 12:40 ASUBUHI
SAA 24 baada ya kutwaa taji la Europa League, wachezaji watatu wa Chelsea, Frank Lampard, Juan Mata na Oscar walikutana na mafanikio zaidi usiku wa jana.
Wakitoka kuifunga Benfica mabao 2-1 katika fainali, nyota hao watatu wa The Blues walishinda pia tuzo za wachezaji bora wa klabu katika vipengele mbalimbali Stamford Bridge.
Mata alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka Chelsea kwa mwaka wa pili mfululizo, Oscar alishinda tuzo ya Bao Bora la Mwaka, Lampard alipewa Tuzo Maalum na chipukizi Nathan Ake alimpiku Mtanzania, Adam Nditi katika tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka.
Tuzo mbili: Juan Mata aliteuliwa Mchezaji Bora wa Mwaka na Mchezaji Bora wa Wachezaji wa Mwaka
Namba Juan: Mata akipokea tuzo ya Mchezaji Bora wa Wachezaji wa Mwaka kutoka kwa John Terry Stamford Bridge
Wana wa Dhahabu: Frank Lampard akipokea tuzo Maalum kutoka kwa Bobby Tambling. Lampard amevunja rekodi ya mabao Chelsea na sasa ndiye mfungaji wa kihistoria wa klabu hiyo.
Kono kubwa: John Terry akimpongeza Oscar kwa kushinda tuzo ya Bao Bora la msimu
Kizazi kijacho: Lampard akimkabidhi Nathan Ake tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Msimu