IMEWEKWA MEI 16, 2013 SAA 2:35 USIKU
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney aliyekuwa katika wiki ngumu, ameishia kwenda kujiliwaza katika viwanja vya gofu na mchezaji mwenzake wa Manchester United, Johnny Evans.
Huku tetesi zikiwa zimeenea kwamba ataondoka na kuhamia Chelsea, Paris,au Madrid, Rooney alikwenda kutuliza kichwa yake katika gofu.
Rooney katika gofu
'WR10', jezi anayovaa Manchester United.
Rooney hakuvaa jezi uwanjani wakati United inapokea taji la ubingwa wa Ligi Kuu kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya Swansea 2-1 Jumapili iliyopita.
Kuna wasiwasi baada ya kukosa nafasi ya kucheza katika mechi ya mwisho ya Sir Alex Ferguson kama kocha United, huenda asipate nafasi nyingine tena ya kutinga uzi wa Mashetani hao Wekundu.
WR10! Rooney na begi lake la gofu
Nguvu: Rooney akimuangalia Johnny Evans akipiga kipira cha gofu
Alex Ferguson akiwa Dante Stakes Day huko York
Sura maarufu: Paul Scholes akiangalia mbio