IMEWEKWA MEI 23, 2013 SAA 6:00 MCHANA
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, amefungiwa mechi moja kwa kufanya fujo na moja kwa kupewa kadi mbili, ya kwanza akipewa mwanzoni mwa mechi.
Ronaldo aliifungia Real bao la kuongoza dakika ya 55 Uwanja wa Bernabeu, lakini Atletico ikasawazisha kupitia kwa Diego Costa kabla ya Joao Miranda kufunga la ushindi dakika za nyongeza.
NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na kocha wake Jose Mourinho wamefungiwa mechi mbili mbili kila mmoja katika Kombe la Hispania kwa matukio waliyofanya katika fainali ya Kombe la Mfalme wakifungwa 2-1 na Atletico.
Kocha Mourinho alipandishwa jukwaani kwa kubishana na marefa juu ya uamuzi, pia mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 50 anaweza kuepuka kuitumia adhabu hiyo kutokana na tangazo la kuondoka kwake Real.
Mfalme wa mabao Real, Ronaldo alipewa kadi nyekundu mwishoni mwa mchezo huo kwa kumpiga tekenahodha wa Atletico, Gabi.
Jose Mourinho akiamriwa kupanda jukwaani na refa Clos Gomez kwenye fainali ya Kombe la Mfalme
Cristiano Ronaldo alitolewa kwa kadi nyekundu dakika za mwishoni kwa kumpiga teke kiungo wa Atletico, Gabi
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, amefungiwa mechi moja kwa kufanya fujo na moja kwa kupewa kadi mbili, ya kwanza akipewa mwanzoni mwa mechi.
Wote watakuwapo kwenye mechi mbili za mwisho za Real La Liga msimu huu - ugenini dhidi ya Real Sociedad Jumapili na nyumbani dhidi ya Osasuna mwishoni mwa wiki itakayofuata- kwa sababu kifungo chao katika Vikombe tu.
La kusawazisha: Atletico wakishangilia bao la kwanza dhidi ya Real
Nahodha wa Atletico, Gabi akiwa ameinua Kombe la Mfalme
Ronaldo aliifungia Real bao la kuongoza dakika ya 55 Uwanja wa Bernabeu, lakini Atletico ikasawazisha kupitia kwa Diego Costa kabla ya Joao Miranda kufunga la ushindi dakika za nyongeza.
Kipigo hicho kutoka kwa mahasimu wao wa Jiji, kinamaanisha Real imemaliza msimu bila taji lolote, wakati Jumatatu ilithibitishwa Mourinho anaondoka.