IMEWEKWA MEI 17, 2013 SAA 1:00 USIKU
KLABU ya Barcelona imesherehekea taji la nne La Liga ndani ya miaka mitano kwa staili ya aina yake usiku wa jana, kwa wachezaji na wapenzi wao kuhudhuria hafla ya chakula cha usiku.
Kikosi kizima kilipambwa na nguo maridadi na viatu vikali, katika kusherehekea taji la 22 la Ligi Kuu ya Hispania katika klabu hiyo, huku wachezaji wanane wa kikosi cha kwanza wakisherehekea taji lao la kwanza la ligi.
Awali klabu hiyo ilifanya maandamano kusherehekea na mashabiki wachezaji wakiwa kwenye mabasi mawili makubw aya wazi juu na kukatiza mitaa ya Jiji Barcelona Jumatatu.
Mvunja rekodi: Lionel Messi akiwasili na mpenzi wake usiku wa jana
Amepona: Eric Abidal amerejea uwanjani mwaka huu baada ya kufanyiwa upasuaji wa ini
Barcelona akwa sasa inaizidi pointi 10 Real Madrid ikiwa imebakiza mechi moja, wakati ligi imebakiza wiki mbili.
Mabeki wa taji: Carles Puyol na Dani Alves
David Villa akiwasili kwenye sherehe za ubingwa Barcelona
Cesc Fabregas na mpenzi wake, Daniella Semaan wakiwasili
Kocha Tito Vilanova akiwasili