// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MZEE TEGETE AWAPA USHINDI YANGA, KHALID ABEID ASEMA SIMBA ITATAFUNA KANDAMBILI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MZEE TEGETE AWAPA USHINDI YANGA, KHALID ABEID ASEMA SIMBA ITATAFUNA KANDAMBILI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, May 17, 2013

    MZEE TEGETE AWAPA USHINDI YANGA, KHALID ABEID ASEMA SIMBA ITATAFUNA KANDAMBILI

    Mzee Tegete akiwa na Jerry Tegete, Oktoba 16, mwaka 2010 mjini Mwanza. Hapa ni baada ya Tegete kuifungia Yanga bao pekee la ushindi dhidi ya Simba dakika ya 70.

    Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA MEI 17, 2013 SAA 12:05 ASUBUHI
    WOTE wa Mwanza Mwanza, John Tegete na Khalid Abeid, lakini wanapishana mapenzi katika timu hizo mbili na utamu zaidi, kuelekea mchezo wa kesho, kila mtu amefagilia upande wake, japo wote kwa maelezo ya kitaalamu, si ya kivivu. 
    Wote wawili walikuwa jukwaani Uwanja wa Nyamagana, Mwanza Agosti 10, mwaka 1974 wakati linapigwa pambano bora zaidi kuwahi kutokea kati ya mapambano ya watani jadi.
    Abeid, japo alikuwa mchezaji wa Simba, kwa sababu alikuwa majeruhi aliingia uwanjani mara moja na kurejea jukwani kuungana na Tegete kushuhudia mchezo huo, ambao Yanga ilishinda 2-1 ikitoka nyuma kwa 1-0 hadi mapumziko.
    Na kuelekea mchezo wa kesho, Tegete ambaye kwa sasa ni kocha wa Toto Africans ya Mwanza, amesema Yanga itashinda, wakati Khalid mfanyabishara anayemiliki kampuni ya Khalid Laundry & Dry Cleaner, amesema Simba SC ndiyo itashinda.
    “Nimecheza na Simba mechi mbili msimu huu na nimechukua pointi nne kwao, nimewapiga Dar es Salaam wamekamilika, na walipokuja hapa Mwanza tukatoka nao sare.
    Na Yanga wametufunga mechi zote msimu huu. Najua kuelekea mchezo huu, timu zote zimefanya maandalizi mazuri, Yanga watabebwa na uzoefu wa wachezaji wake. Hii ni mechi kubwa, Simba SC wachezaji wake wengi wachanga, mimi kwa kweli nawapa nafasi kubwa sana Yanga kushinda hii mechi,”. Hayo ni maneno ya Mzee Tegete alipozungumza na BIN ZUBEIRY jana kwa simu kutoka Mwanza.
    “Mimi katika mechi hii, nawapa nafasi kubwa sana Simba SC kushinda. Kitakachowaangusha Yanga SC ni kujiamini kupita kiasi, wao wanaona wana timu bora sana kuliko Simba. Kweli, Simba wana vijana wadogo, lakini wale vijana mimi nawapa nafasi ya kuwafunga Yanga.
    Tena nikuambie, katika miaka ya karibuni, mimi sijawahi kuvutiwa na mechi za Simba na Yanga, ila hii imenivutia sana na nina hamu nayo, kwa sababu naamini Yanga wanafungwa na wale watoto,”. Hayo ni maneno ya Khalid Abeid, kiungo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, alipozugumza n BIN ZUBEIRY jana.
    Je, nani ametabiri sahihi kati yao? Bila shaka ni jambo la kusubiri na kuona baada ya dakika 90 kesho. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MZEE TEGETE AWAPA USHINDI YANGA, KHALID ABEID ASEMA SIMBA ITATAFUNA KANDAMBILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top