IMEWEKWA MEI 22, 2013 SAA 12:45
KLABU za Real Madrid na Barcelona zinamtaka beki wa kati wa Chelsea, David Luiz.
Mbrazil huyo anaweza kuwa lulu mbele ya kocha mpya anayekuja, Jose Mourinho ambaye amevutiwa na uwezo wake katika nafasi ya ulinzi.
KLABU za Real Madrid na Barcelona zinamtaka beki wa kati wa Chelsea, David Luiz.
Mbrazil huyo anaweza kuwa lulu mbele ya kocha mpya anayekuja, Jose Mourinho ambaye amevutiwa na uwezo wake katika nafasi ya ulinzi.
Luiz aliigharimu Chelsea Pauni Milioni 21 nna watataka faida ikibidi kuuuza bidhaa hiyo waliyoinunua mwaka 2011.
Mpiganaji: Beki wa Chelsea, David Luiz alisajiliwa kwa Pauni Milioni 21 kutoka Benfica
Nyota: Luiz alikuwa na mchango mkubwa wakati Chelsea inatwaa Europa League
Mourinho anataka beki mpya wa kati, kiungo mkabaji na angalau mshambuliaji mmoja katika kurejea kwake Stamford Bridge. Luiz amekuwa akitumika kama kiungo mkabaji chini ya Rafa Benitez na imemsaidia kupunguza makosa yake wakati anacheza kama beki.
Chelsea imeonyesha nia ya kumsajili mchezaji anayetakiwa na Liverpool, Krygiakos Papadopoulos wa Schalke, lakini inamchukulia kinda huyo wa miaka 21 kama ghali sana. Mourinho ni shabiki mkubwa wa Raphael Varane wa Real Madrid pia, lakini suala hilo litaingiliwa na siasa zake za kuondoka Bernabeu.
Tayari, wanaonekana kuimarisha safu yao ya ulinzi wakiwa na Branislav Ivanovic ambaye pia anawezwa kuhamishiwa beki ya kulia.
Kipaji: Raphael Varane wa Real Madrid (akipiga juu) anakubalika mno mbele ya Mourinho
Kazi ya kwanza ya Jose Mourinho Chelsea itakuwa kuimarisha safu ya ulinzi
Madrid itakijenga upya kikosi cha Mourinho kupitia kwa Carlo Ancelotti. Watakuwa tayari kumuuza beki Pepe kuliko Varane na Manchester City wamepewa ofa ya kumsajili beki huyo Mreno kwa Pauni Milioni 20.
Kwa upande wao, Barcelona wanapambana kuwania saini ya beki wa kati ambaye hatazidi Pauni Milioni 25. Luiz yumo kwenye orodha yao muda mrefu, lakini si kipaumbele cha mwanzoni.
Mourinho atatakiwa kuamua mustakabali wa John Terry na Frank Lampard msimu ujao
Walimtaka Thiago Silva kutoka Paris St Germain, lakini ni ghali mno wakati Manchester City hawako tayari kumuuza Vincent Kompany. Barca inamtaka beki kinda wa Roma, Marquinhos lakini anaweza kuwa tayari kubaki kwa msimu mwingine Italia.
Thomas Vermaelen wa Arsenal anaweza kurejesha makali yake, lakini kumaliza kwake msimu vibaya kunamfanya Luiz awe midomoni mwa watu zaidi yake.
Vincent Kompany kushoto na Thiago Silva kulia
Thomas Vermaelen amekuwa akimulikwa na Chelsea