IMEWEKWA MEI 24, 2013 SAA 4:55 ASUBUHI
KATIKA mahojiano yaliyochapishwa England asubuhi ya leo, Mtendaji Mkuu wa Manchester City, Ferran Soriano amesema klabu yake itakuwa ikicheza soka ya kuvutia na ya ushindi.
Ikiwa Marekani, imeweza kufanya yote hayo leo ikicheza mechi ya kirafiki na Chelsea kwa kutoka nyuma kwa mabao matatu na kuibuka na ushindi wa kuburudisha kwenye Uwanja wa St Louis Cardinals, Busch.
Kusema kwamba City – inayofundishwa na Brian Kidd baada ya kufukuzwa kwa Roberto Mancini ilikuwa timu bora hapa itakuwa ni kuishusha thamani. Walicheza soka ya kuvutia mbele ya mashabiki 48,263, hususan katika kipindi cha kwanza, na wakitengeneza nafasi kibao nzuri ndani ya dakika zote 90. Lakini Chelsea ilitangulia kupata mabao yake kupitia kwa Ba dakika ya 14, Azpilicueta dakika ya 45 kwa penalti na Oscar dakika ya 53.
Manchester City ikasawazisha kupitia kwa Garcia dakika ya 63, Dzeko dakika ya 64 na 85 na beki aliyekuwa anarejea uwanjani baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kwa sababu ya majeruhi, Richards akafunga la ushindi dakika ya 90.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa;
Cech/Blackman dk61, Azpilicueta/Ferreira dk45, Ivanovic/Luiz dk45, Cahill/Ramires dk45, Christensen, Mikel, Mata/Oscar dk45, Benayoun, Loftus-Cheek/Ake dk80, Cole na Ba/Torres dk45.
Man City: Hart/Wright dk45, Zabaleta/Maicon dk62, Kompany/Richards dk45, Rekik/Boyata dk80, Clichy, Garcia, Yaya Toure/Huws dk45, Rusnak/Milner dk62, Tevez, Silva/Nasri dk45 na Aguero/Dzeko dk45.
Bao la ushindi: Micah Richards kushoto aliifungia Man City bao la ushindi dhidi ya Chelsea
Demba Ba akiifungia Chelsea bao la kuongoza
Bao la tatu la Chelsea