// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LAMPARD AINUSURU ENGLAND KULALA NYUMBANI MBELE YA IRELAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LAMPARD AINUSURU ENGLAND KULALA NYUMBANI MBELE YA IRELAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Thursday, May 30, 2013

        LAMPARD AINUSURU ENGLAND KULALA NYUMBANI MBELE YA IRELAND

        IMEWEKWA MEI 29, 2013 SAA 5:55 USIKU
        ENGLAND imetoka sare ya 1-1 na Jamhuri ya Ireland katika mchezo wa kirafiki usiku kwenye Uwanja wa Wembley.Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa William Collum wa Scotland, Ireland ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao ugenini, mfungaji Shane Long dakika ya 13, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Seamus Coleman kutoka wingi ya kulia.
        Frank Lampard aliwasawazishia wenyeji dakika 10 baadaye, yaani dakika ya 23 kuftaia kazi nzuri ya Daniel Sturridge ambaye aliambaa uipande wa kushoto wa box, kabla ya kummiminia krosi mfungaji, aliyemtungua kipa Glenn Whelan.
        Ashley Cole alipewa kofia ya dhahabu baada ya kutimiza mechi 100 za timu ya taifa ya England leo. 
        Katika mchezo huo, kikosi cha England kilikuwa: Hart/Foster dk46, Johnson/Jones dk46, Cahill, Jagielka, Cole/Baines dkl54, Walcott, Lampard, Carrick, Oxlade-Chamberlain/Milner dk87, Rooney na Sturridge/Defoe dk33.
        Ireland: Forde, Coleman, O'Shea, St. Ledger, Kelly, Walters/Sammon dk82, McCarthy, Whelan/Hendrick dk74, McGeady/McClean dk68, Long na Keane/Cox dk66.
        Level terms: Frank Lampard (right) pokes home the equaliser for England
        Mwokozi; Frank Lampard aliifungia England bao la kusawazishaHeads I win: Shane Long nods Republic of Ireland ahead at Wembley against England

        Furaha: Shane Long akishangilia bao lake
        Tonderful: Roy Hodgson presents Ashley Cole with a golden cap to mark 100 appearances for England
        Roy Hodgson akimkabidhi Ashley Cole kofia ya dhahabu kwa kutimiza mechi 100 England
        On the slide: Ireland's Stephen Kelly makes a tackle on England's Theo Walcott
        Stephen Kelly wa Ireland akimdhibiti Theo Walcott wa England
        Off target: Wayne Rooney lobs a shot wide of the goal for England
        Wayne Rooney akipiga shuti lililopaa
        Getting shirty: England captain Ashley Cole sees his shirt pulled by Irleand's Seamus Coleman
        Nahodha wa England, Ashley Cole akivutwa jezi na Seamus Coleman wa Ireland
        Taking a tumble: Ireland's Shane Long and England's Gary Cahill battle for an aerial ball
        Shane Long wa Ireland akipambana na Gary Cahill wa England
        Level terms: Frank Lampard (right) pokes home the equaliser for England
        Frank Lampard (kulia) akiisawazishia England
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments
        Item Reviewed: LAMPARD AINUSURU ENGLAND KULALA NYUMBANI MBELE YA IRELAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry