// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HANS POPPE; VIJANA WAMETUAHIDI KUTAFUNA KANDAMBILI TAIFA KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HANS POPPE; VIJANA WAMETUAHIDI KUTAFUNA KANDAMBILI TAIFA KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, May 17, 2013

    HANS POPPE; VIJANA WAMETUAHIDI KUTAFUNA KANDAMBILI TAIFA KESHO

    Furaha mapema; Hans Poppe amesema vijana wameahidi kutafuna kandambili kesho

    Na Prince Akbar, IMEWEKWA MEI 16, 2013 SAA 12:01 ASUBUHI
    WACHEZAJI wa Simba SC wamewaahidi Friends of Simba kwamba kesho wataifunga Yanga SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na hakuna shaka juu ya hilo.
    “Tumezungumza na vijana, tumewatembelea hapa kambini, wako vizuri na wametuhakikishia Jumamosi wanamnyoa Yanga akashangilie ubingwa chumbani kwake, si mbele yao,”alisema Mwenyekiti wa Friends of Simba, alipozungumza na BIN ZUBEIRY jana usiku.
    Hans Poppe alisema kuhusu wamewaandalia nini iwapo watashinda mechi hiyo, watawaambia wakifika Dar es Salaam. “Bahasha ya ahadi ya bakhshishi yao tutawafungulia watakapotua Dar es Salaam kutoka Zanzibar (kesho) saa chache kabla ya kwenda uwanjani,”alisema Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ). 
    Simba SC imeweka kambi maeneo ya Mbweni, Zanzibar ikifanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Mao Dze Tung katikati ya mjini huo wa kitalii. 
    Mchezo wa kesho unatarajiwa kuchezeshwa na refa Martin Saanya kutoka Morogoro, akisaidiwa na Samuel Mpenzu wa Arusha na Jesse Erasmo kutoka Morogoro, wakati refa akiba atakuwa ni Hashim Abdallah wa Dar es Salaam.
    Kamisaa wa mechi hiyo atakuwa Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya wakati mtathmini wa waamuzi atakuwa ni Leslie Liunda wa Dar es Salaam.
    Mashabiki watakaotaka kwenda kushuhudia mpambano huo wa mahasimu wa jadi katika soka ya Tanzania, watalazimika kulipa Sh. 5,000, hicho kikiwa kiingilio cha chini zaidi katika sehemu ya viti vya Rangi ya Bluu. 
    Aidha, katika mchezo huo utakaoanza saa 10:00 jioni, viingilio vingine ‘nafuu kidogo’ vitakuwa ni Sh 7,000 kwa viti ya Rangi ya Kijani na Sh. 10,000 kwa viti vya Rangi ya Chungwa.
    Upande wa ‘wakubwa’, viingilio vitakuwa ni Sh. 15,000 kwa VIP C, Sh. 20,000 kwa VIP B na Sh. 30,000 kwa VIP A na tiketi zitaanza kuuzwa kesho.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: HANS POPPE; VIJANA WAMETUAHIDI KUTAFUNA KANDAMBILI TAIFA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top