IMEWEKWA MEI 16, 2013 SAA 2:33 USIKU
KIUNGO David Beckham amesstaafu soka akiwa na umri wa miaka 38, uamuzi ambao ameutangaza rasmi leo.
Nahodha huyo wa zamani wa England, anayekwenda kwa jina la utani 'Mipira ya Dhahabu', atatungika daluga zake baada ya kunyanyua taji lingine la ligi ya Ufaransa akiwa na Paris St Germain.
Beckham ameamua kustaafu na sasa ataelekeza muda wake mwingi kwa mkewe Victoria na watoto wake wanne, mdogo kabisa ni Harper, mwenye miezi 21 tangu kuzaliwa.
Beckham amesema katika taarifa yake iliyoifikia BIN ZUBEIRY leo kwamba: "Nawashukuru PSG kwa kunipa nafasi ya kuendelea, lakini nafikiri sasa ni wakati mwafaka kumaliza, nimecheza katika kiwango cha juu,".
Hisia: David Beckham akizungumzia kustaafu kwake soka baada ya miaka 21
Mwisho wa zama: Beckham amesema; "Naupenda sana mchezo - Nafikiri na wakati mwafaka kuondoka'
Mtu wa wakati: David Beckham, katika picha aliyopigwa akiwa kwenye viwanja vya mazoezi vya Paris Saint Germain leo akitangaza kustaafu