// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BABA NGASSA ATOA BARAKA ZOTE MWANAWE KUREJEA YANGA, ASEMA "KIJANA AMEKUA, ANAJIAMULIA" - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BABA NGASSA ATOA BARAKA ZOTE MWANAWE KUREJEA YANGA, ASEMA "KIJANA AMEKUA, ANAJIAMULIA" - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, May 20, 2013

    BABA NGASSA ATOA BARAKA ZOTE MWANAWE KUREJEA YANGA, ASEMA "KIJANA AMEKUA, ANAJIAMULIA"

    Baba yake Mrisho, Mzee Khalfan Ngassa 'Babu' kulia akiwa na BIN ZUBEIRY leo Dar es Salaam

    Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA MEI 20, 2013 SAA 11:10 JIONI
    WAKATI baba Mrisho Ngassa, Mzee Khalfan Ngassa ‘Babu’ ametoa Baraka zote mwanawe kurejea Yanga SC, kijana wake huyo amesema kwamba kutoaminiwa wakati wote ndani ya Simba SC ndiko kumemshinikiza kurejea klabu yake ya zamani, ambayo amekiri ipo ndani ya damu yake.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo, kwa upande wake Babu Ngassa alisema; “Mwanangu sasa ni mtu mzima, ana umri zaidi ya miaka 18, ana uhuru wa kujiamulia mambo, hivyo sina kipingamizi na uamuzi wake wa kurejea Yanga na ninatoa Baraka zote.
    Ninamtakia kila la heri mwanangu, aendelee kuwa mchezaji mwenye mafanikio katika soka ya Tanzania na siku moja atomize ndoto zake zaidi na zaidi,”alisema Ngassa, ambaye naye amewahi kuchezea Simba SC mwaka 1990 na 1991 akitokea Pamba FC ya Mwanza.
    Mrisho Ngassa akisani kitabu maalum baada ya kurejea Yanga, Jangwani leo

    Ngassa mwenyewe amesema kwa muda mrefu amekuwa akizushiwa amesaini Yanga, lakini ukweli ni kwamba hakuwa amesaini ila baada ya kuona haaminiwi kabisa ndani ya Simba SC akaona bora aende kule ambako ataaminiwa.
    “Ni kweli mimi naipenda Yanga, lakini wakati nikiwa nacheza Simba nilikuwa nacheza kwa kujituma na kujitolea na kila mtu alikuwa anaona mchango wangu. Mimi naheshimu mpira kwa sababu ni kazi yangu, siwezi kuvuruga,”alisema.
    Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb amempongeza Ngassa kwa kuwa mchezaji mfano wa kuigwa kwa wachezaji wanaoheshimu kazi yao.
    “Huyu kijana tumekuwa katika mazungumzo naye kumrejesha hapa kwa muda mrefu, miezi sita sasa, lakini siku zote aliendelea kuitumikia Simba SC na hadi juzi yeye ndiye aliyesababisha penalti ya Simba wakakosa. Kwa kweli tunajivunia kumrudisha hapa huyu kijana,”alisema Bin Kleb.  
    Ngassa amesaini mkataba wa miaka miwili Yanga SC na ametambulishwa rasmi leo asubuhi makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
    Ngassa aliichezea Simba SC mechi ya 27 na ya mwisho Jumamosi katika kipindi cha kuwa kazini Msimbazi, wakati ilala mabao 2-0 mbele ya Yanga.
    Siku hiyo, Ngassa aliwajibika vizuri akiisaidia Simba SC kupata penalti dakika ya 27, baada ya kuangushwa kwenye eneo la hatari na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, wakati huo Yanga inaongoza 1-0, lakini Mussa Mudde akapoteza nafasi ya kuisawazishia timu yake kwa mkwaju wake kuokolewa na Ally Mustafa ‘Barthez’.
    Katika mechi 27 alizoichezea Simba SC, zikiwemo za Ligi ya Mabingwa mbili, kirafiki kadhaa na Ligi Kuu, Ngassa amefunga jumla ya mabao saba na kutoa pasi za mabao 13.
    Baada ya mechi dhidi ya Yanga Jumamosi, mashabiki wa timu ya Jangwani walimfuata Ngassa na kumvalisha jezi ya timu hiyo, jambo ambalo liliwakera mashabiki wa Simba SC.
    Ngassa alitua Simba SC kwa mkopo Agosti mwaka jana akitokea Azam FC ya Dar es Salaam pia, ambayo nayo iliamua kumtoa kundini baada ya kukerwa na ‘Uyanga wake’.
    Ngassa alifunga bao la pili na la ushindi dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dakika za lala salama katika Nusu Fainali ya Kombe la Kagame Uwanja Taifa, Dar es Salaam na kwenda kushangilia kwa kuibusu jezi ya Yanga, jambo ambalo liliwakera Azam na wakatangaza kumuuza.
    Hata hivyo, Simba SC ilifanikiwa kuipiku Yanga SC kwa kuuziwa mchezaji huyo kwa Sh. Milioni 25 kwa mkopo. Lakini alipotua Simba SC, ikaelezwa aliongeza mkataba wa mwaka mmoja na kupewa Sh. Milioni 30, kati ya hizo Milioni 12 fedha taslimu na Milioni 18, thamani ya gari aina ya Verosa.  
    Lakini Ngassa mwenyewe alisema alipewa Milioni hizo 30 ili akubali kushuka Msimbazi na si kusaini mkataba mpya. 
    Ngassa alisajiliwa Azam Mei 21, mwaka 2010, kwa dola za Kimarekani 40,000, zaidi ya Sh. Milioni 60 kutoka Yanga SC, huku yeye mwenyewe akipewa dola 30,000, zaidi ya Sh. Milioni 45. 
    Alitua Yanga kwa mara ya kwanza mwaka 2006, akitokea Kagera Sugar ya Bukoba, ambayo ilimtoa Toto African ya Mwanza.
    Aprili mwaka 2009, Ngassa alifanya majaribio katika klabu ya West Ham United ya England wakati huo ipo chini ya kocha Mtaliano, Gianfranco Zola, ambako pamoja na kuvutia lakini akaambiwa ‘lishe ndogo’.
    Aliwahi pia kufanya majaribio Seattle Sounders FC ya Marekani na akapewa nafasi ya kucheza kwa dakika nane akitokea benchi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Manchester United na siku hiyo alikaribia kufunga pamoja na kumuumiza beki Rio Ferdinand. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BABA NGASSA ATOA BARAKA ZOTE MWANAWE KUREJEA YANGA, ASEMA "KIJANA AMEKUA, ANAJIAMULIA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top