IMEWEKWA MEI 25, 2013 SAA 12:50 ASUBUHI
KLABU ya Arsenal wanajipanga kubomoa benki ili kumsajili mshambuliaji Wayne Rooney.
Kutoka Sportmail BIN ZUBEIRY inafahamu kwamba The Gunners iliibua nia thabiti ya kumsajili nyota huyo anayetaka kuondoka Manchester United wiki iliyopita.
Mpango wa kumsajili Rooney ulijadiliwa kwa mara ya kwanza katika kikao cha usajili cha Machi, lakini kipingamizi kikawa mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki utakuwa mzigo mzito kwa klabu hiyo.
Ataondoka? Wayne Rooney inaaminika anataka kuondoka Old Trafford
Pamoja na hayo, Arsenal ikaamua kutoachana na mpango wa kumsajili Rooney kwa ajili ya msimu ujao. Amebakiza miaka miwili katika mkataba wake Old Trafford, na The Gunners wanatumai kwamba ofa ya mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki itamvutia mshambuliaji huyo.
Arsenal pia iko tayari kutoa mamilioni ya Pauni kwa ajili ya kumnasa Rooney mbali ya mshahara wake.
Arsenal pia iko tayari kutoa mamilioni ya Pauni kwa ajili ya kumnasa Rooney mbali ya mshahara wake.
Dili hilo litamfanya Rooney awe mchezaji anayelipwa zaidi kihistoria katika klabu hiyo.
Lukas Podolski na Theo Walcott kwa sasa ndio wachezaji wanaolipwa zaidi Arsenal, kiasi cha Pauni 100,000 kwa wiki. Lakini Ofisa Mtendaji Mkuu aliyeondoka wa United, David Gill bado anataraji Rooney atauanza msimu mpya na mabingwa hao wa Ligi Kuu licha ya nia ya Arsenal kumsajili.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa akihusishwa na kuondoka Old Trafford baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson — ambaye nafasi yake imechukuliwa na kocha wa Everton, David Moyes — aliyesema Rooney ametoa maombi ya kuondoka kwa mara ya pili ndani ya wiki tatu.
Mtu wa kwanza: Rooney amelazimika kuwa chaguo la pili tangu kuwasili kwa Robin van Persie kutoka Arsenal
Lakini Gill anasema: "Nafikiri huyo ni babu kubwa, mchezaji mkubwa katika klabu kubwa na klabu haitaki kumpoteza mchezaji wake nyota,".
"Nina uhakika kila jitihada inafanyika kwa Wayne na washauri wake kuhakikiksha inakuwa hivyo. Mimi si mtu wa kucheza kamari, lakini naamini nitakaa Old Trafford msimu ujao na kumuona Wayne Rooney akifanya vitu vyake,"alisema Gill.
Mzaliwa huyo wa Liverpool, Rooney alisaini mkataba wa miaka mitano unaomalizika Juni 2015 baada ya kughairi mpango wake wa kuihama klabu hiyo Oktoba 2010.