FADHILA nzuri ambazo kocha Arsene Wenger anaweza kulipa kwa Robin van Persie ilikuwa ni kumfananisha na mwanamke aliyechelewa kupata mtoto hadi umri wa miaka 39.
Si hivyo tu, lakini Wenger hafikirii kama nyota huyo mwenye mabao 24 anastahili tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA na Michael Carrick ndiye chaguo la kocha huyo wa Arsenal.
"Wakati fulani si tu mfungaji apewe tuzo, bali mchezaji halisi katika moyo wa mchezo,"alisema Wenger, ambaye amesema watawapa heshima yao Manchester United katika mchezo wa kesho.
Hasira: Robin van Persie hajapata mafanikio akiwa Arsenal kwa miaka kadhaa
"Carrick, kwangu, anastahili hii. Anatoa pasi bora. Anaweza kucheza Barcelona. Anaweza kuendana na mchezo wao."
Van Persie kesho atarejea Arsenal kwa mara ya kwanza tangu ahamie Old Trafford. Matunda ya kuondoka kwake Arsenal na kutua United yameanza kuonekana baada ya kuiwezesha timu hiyo kurudisha ubingwa wa Ligi Kuu.
Chuki? Arsene Wenger amesema Van Persie hastahili kuwa mchezaji bora wa mwaka
Alipoulizwa kama alijua Van Persie atakwenda 'kulipa' Old Trafford, Wenger alionekana kuhamaki, kabla ya kusema: "Ndiyo! Tusingeweza kushindana kwa sababu ilikuwa imekwishakaa vibaya.
"Ni kijana mkweli, Robin. Amefikisha miaka 29 na alifikiri, “Tunaweza kutwaa ubingwa hapa au ninaweza kuwa na nafasi sehemu nyingine pia?” Kuna wakati mgumu kama ambao anaweza kukutana nao mwanamke ambaye katika umri wa miaka 39 hajapata mtoto. Ataanza kufikiri, “Sina muda zaidi”.’