KLABU ya Liverpool inafikiri kifungo cha mechi 10 cha Luis Suarez kwa kumng'ata Branislav Ivanovic kinaweza kumlazimihsa kuondoka England.
Klabu hiyo Anfield ilishitushwa na kupatwa mfadhaiko juu ya adhabu kali ya Suarez na ina wasiwasi mshambuliaji huyo wa Uruguay atahisi hana chaguo lingine zaidi ya kuhama mwishoni mwa msimu.
Amekuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa na kuhamia klabu za Bayern Munich, Paris Saint-Germain na Juventus, na sasa anaweza kuzungumzia mipango hiyo na wakala wake, Pere Guardiola — kaka wa kocha ajaye Bayern, Pep — na wanasheria wake.
Nimerudi: Luis Suarez amerejea mazoezini jana huku FA ikimpa adhabu kali
Suarez mazoezini na Liverpool, hapa akichuana na Dan Agger
Nyama mbichi: Suarez akimng'ata Branislav Ivanovic katika mechi ya Ligi Kuu England Uwanja wa Anfield
Liverpool inasistiza inamtaka Suarez abaki Merseyside kumalizia mkataba wake wa miaka minne.
Lakini wanaweza kumuacha kijana huyo mwenye umri wa miaka 26 aondoke kama anafikiri hatendewi haki.
Suarez anaweza kukata rufaa lakini, Jumatano, Mwenyekiti wa klabu ya mashabiki wa Liverpool alimtaka akae kimya, akubaliane na adhabu.
Akionyesha mfano: Refa Kevin Friend, akionyeshwa na Ivanovic alivyong'atwa na Suarez
ADHABU YAKE INAFANANISHWA NA ZA AKINA NANI?
MIEZI TISA
Eric Cantona (Manchester United): kwa kumpiga teke la ‘kung-fu' shabiki wa Crystal Palace mwaka 1995
Mark Bosnich (Chelsea): baada ya vipimo kuthibitisha anatumia cocaine mwaka 2003
Mark Bosnich (Chelsea): baada ya vipimo kuthibitisha anatumia cocaine mwaka 2003
MIEZI NANE
Rio Ferdinand (Manchester United): Kutotokea kwenye vipimo vya dawa za kulevya mwaka 2003
MECHI 12
Duncan Ferguson (Rangers): Kumpiga teke la kichwa John McStay wa Raith mwaka 1994
Joey Barton (QPR): Kufanya vurugu baada ya kutolewa nje mwaka 2012
Joey Barton (QPR): Kufanya vurugu baada ya kutolewa nje mwaka 2012
MECHI 11
Paolo Di Canio (Sheffield Wednesday): kumsukuma refa Paul Alcock mwaka 1998
MECHI 10
Kevin Keegan (Liverpool) na Billy Bremner (Leeds): kwa kupigana kwenye mechi ya Ngao mwaka 1974
David Prutton (Southampton): kumsukuma refa Alan Wiley mwaka 2005
David Prutton (Southampton): kumsukuma refa Alan Wiley mwaka 2005
MECHI TISA
Paul Davis (Arsenal): kumsukuma Glenn Cockerill mwaka 1998MECHI NANE
Luis Suarez (Liverpool): Hila za kibnaguzi kwa Patrice Evra mwaka 2011
MECHI TANO
Roy Keane (Man United): kukiri alimuumiza Alf-Inge Haaland wa Man City
Kifungo hicho kitamfanya mchezaji huyo akae benchi katika mashindano ya ndani hadi Septemba — ingawa atakuwa huru kuichezea Uruguay katika Kombe la Mabara Juni — lakini ana muda wa kuamua mchana wa leo kama atakata rufaa dhidi ya adhabu hiyo.
Na taarifa ya FA imesema: "Luis Suarez amesimamishwa kwa mechi 10 baada ya kikao cha kamati ya kanuni kumkuta na hatia.
"(Wao) waliona adhabu ya mechi tatu ya FA haitatosha kwa kitendo hicho na mchezaji huyo alihitaji kufungiwa mechi saba zaidi.
"Adhabu inaanza mara moja.
Liverpool itaendeela kusimama upande wa Suarez, na licha ya hatua alizochukua ni yeye atakayeamua kukata rufaa na amewahidiwa sapoti ya kutosha.
Tayari wana tahadhari, wakipoteza rufaa wanaweza kushuhudia Suarez akiongezewa adhabu.
Wakati nyota huyo wa Uruguay alipofungiwa mechi saba baada ya kumng'ata kiungo wa PSV Eindhoven, Otman Bakkal Novemba 2010, hakupambana na adhabu hiyo iliyotolewa na Ajax na FA ya Uholanzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Liverpool, Ian Ayre amesema: "Wote klabu na mchezaji tumeshitushwa na kufadhaishwa na hatua ya Kamati ya Kanuni.
Tunasubiri sababu za kimaandishi kabla ya kuzungumzia zaidi,".
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers hajazungumzia hadharani tatizo hilo tangu baada ya sare ya 2-2 Jumapili dhidi ya Chelsea lakini anatarajiwa kuzungumza na Waandishi wa Habari leo.
Mfuate: Suarez akigombana na Patrice Evra mwaka 2011 ambayo ilimfanya afungiwe mechi nane
'JELA ALIZOSWEKWA' SUAREZ LIVERPOOL
MECHI 10...
Kumng'ata Branislav Ivanovic - Aprili 24, 2013
Kumng'ata Branislav Ivanovic - Aprili 24, 2013
MECHI 8...
Hila za kibaguzi kwa Patrice Evra - Desemba 20, 2011
Hila za kibaguzi kwa Patrice Evra - Desemba 20, 2011
MECHI 1...
Kadi tano za njano - Desemba 1, 2012
Kadi tano za njano - Desemba 1, 2012
MECHI 1...
Kushangilia kwa kebehi mbele ya mashabiki wa Fulham - Desemba 5, 2011
Kushangilia kwa kebehi mbele ya mashabiki wa Fulham - Desemba 5, 2011
JUMLA YA KIFUNGO: Mechi 20