// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WAMOROCCO WATUA NA VISA...NYODO KWA WINGIIIIIII, ETI WAGOMEA HOTELI AMBAYO WAPINZANI WOTE WA AZAM WALILALA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WAMOROCCO WATUA NA VISA...NYODO KWA WINGIIIIIII, ETI WAGOMEA HOTELI AMBAYO WAPINZANI WOTE WA AZAM WALILALA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, April 18, 2013

    WAMOROCCO WATUA NA VISA...NYODO KWA WINGIIIIIII, ETI WAGOMEA HOTELI AMBAYO WAPINZANI WOTE WA AZAM WALILALA

    Wazee wa visa; AS FAR Rabat

    Na Prince Akbar
    VISA. Vituko mapemaaa. Wapinzani wa Azam FC katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, AS FAR Rabat ya Morocco wamewasili jana Dar es Salaam lakini wakafanya vituko hivyo, we acha tu.
    Kwanza walikuwa ni watu wenye wasiwasi tangu wanatua Uwanja wa Ndege na wasiowaamini wenyeji wao, wakitaka zaidi kujiongoza wenyewe na baadaye sasa wakakataa hoteli waliyokodiwa na wenyeji wao, Sapphire Court.
    Pamoja na kuambiwa hoteli hiyo imepitishwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na timu zote zilizocheza na Azam katika mashindano hayo, zilifikia hapo, Al Nasir ya Sudan Kusini na Barack Young Controllers II ya Liberia, lakini wakagoma.
    Wenyeji wakawaambia kama hawataki hoteli hiyo watajilipia popote watakapokwenda na Waarabu hao nao wakaonyesha jeuri ya fedha kwa kujipangia New Africa Hotel. Kaazi kweli kweli.
    Lakini hizi ni dalili mbaya kwa Waarabu hao kugomea hoteli na visa vyote walivyofanya, kuna hatari Azam wakafanyiwa visa zaidi watakapokwena Morocco kwa ajili ya mchezo wa marudiano.
    Azam itamenyana na Waarabu hao Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Tatu, kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye Morocco na mshindi wa jumla ataingia kwenye droo ya kucheza na timu zilizotolewa katika Ligi ya Mabingwa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho. 
    Azam FC ilifanikiwa kuingia Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, baada ya kuifunga jumla ya mabao 2-1 Barack Young Contollers II ya Liberia.
    Ilianza kwa kushinda 2-1 mjini Monrovia kabla ya kulazimishwa sare ya bila kufungana Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: WAMOROCCO WATUA NA VISA...NYODO KWA WINGIIIIIII, ETI WAGOMEA HOTELI AMBAYO WAPINZANI WOTE WA AZAM WALILALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top