MSHAMBULIAJI Wayne Rooney ndiye mchezaji tajiri zaidi katika Ligi Kuu ya England akiwa anaingiza kipato cha Pauni Milioni 51, kwa mujibu wa orodha ya matajiri katika gazeti la Sunday Times la Uingereza.
Mshambuliaji huyo ambaye mshahara wake umeongezeka hadi Pauni Milioni 45 mwaka jana, anamzidi kwa Pauni Milioni 9 mchezaji mwenzake wa Manchester United, Ferdinand.
Rooney na mkewe Colleen kwa pamoja utajiri wao ni Pauni Milioni 64.
Yuko juu: Wayne Rooney ndiye tajiri zaidi katika wachezaji wa Ligi Kuu England katika orodha inayoongozwa na David Beckham (chini)
Mshambuliaji huyo na beki huyo wa kati, Ferdinand ni wawili miongoni mwa wachezaji 24 wa Ligi Kuu England hivi sasa kwenye orodha ya wanamichezo 100 matajiri Uingereza na Ireland, kwa mujibu wa orodha iliyochapishwa leo.
David Beckham anaongoza kwa utajiri wenye thamani ya Pauni Milioni 165 jumla.
Michael Owen (Pauni Milioni 38) anashika nafasi ya tatu, mbele ya Ryan Giggs na Frank Lampard (wote Pauni Milioni 34).
Wachezaji sita wa Manchester United wamo kwenye orodha hiyo, wakiwemo Paul Scholes, Michael Carrick na Robin van Persie, ambao ni ingizo jipya wakiwa na utajiri wa Pauni Milioni 12.
Michael Carrick (kushoto) na Frank Lampard (kulia) nao wamo
Steven Gerrard ndiye mchezaji tajiri zaidi Liverpool akiwa na Pauni Milioni 33, huku Carlos Tevez (Pauni Milioni 18) ndiye tajiri zaidi kwa upande wa wachezaji wa Manchester City.
Nahodha wa zamani wa England, Beckham, anayechezea Paris St Germain, pamoja na kuwa mchezaji tajiri zaidi Uingereza, anashika nafasi ya 11 katika orosha ya jumla ya wachezaji matajiri duniani, inayoongozwa na mcheza gofu, Tiger Woods, mwenye Pauni Milioni 570.
Kwa pamoja Beckham na utajiri wa mkewe, Victoria wana Pauni Milioni 200.
Kuna wanasoka wengine wawili 20 Bora ya wanamichezo matajiri duniani, ambao ni nyota wa Barcelona, Lionel Messi, mwenye Pauni Milioni 125 na mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, mwenye Pauni Milioni 120.
Tathmini ya utajiri wa wanamichezo hawa, imetokana na mali wanazomiliki, ikiwemo ardhi, mali zisizohamishika na rasilimali nyingine pamoja na akaunti zao za benki.
United matajiri: Wachezaji wenzake sita Rooney wamo kwenye orodha, akiwemo Rio Ferdinand na Robin van Persie