// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); VIBONDE WA AZAM WAJA KESHO DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE VIBONDE WA AZAM WAJA KESHO DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, April 01, 2013

    VIBONDE WA AZAM WAJA KESHO DAR

    Azam FC; Vibonde wao waja kesho

    Na Boniface Wambura
    KLABU ya Barrack Young Controllers II ya Liberia inatarajia kuwasili nchini kesho kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji Azam itakayochezwa Jumamosi wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Young Controllers itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 3.35 asubuhi kwa ndege ya PrecisionAir ikitokea Nairobi, Kenya inapounganisha safari hiyo inayoanzia Monrovia kupitia Accra, Ghana.
    Msafara wa timu hiyo utakuwa na watu 37 wakiwemo wachezaji 21 na utaongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo, Robert Alvin Sirleaf ambaye ni mtoto wa Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf.
    Wachezaji waliomo kwenye kikosi hicho ni Abraham Andrew, Alfred Hargraves, Alpha Jalloh, Benjamin Gbamy, Cammue Tumamie, Erastu Wee, Ezekiel Doe, George Dauda, Hilton Varney, Ishmail Paasewe, Joekie Solo, Joseph Broh, Junior Barshall, Karleo Anderson, Mark Paye, Prince Jetoh, Prince Kennedy, Randy Dukuly, Raymond Blamonh na Winston Sayou.
    Benchi la ufundi linaongozwa na Kocha Mkuu, Robert Lartey akisaidiwa na Samuel Sumo wakati Meneja wa timu ni Clarence Murvee. Daktari wa timu ni Samuel Massaquoi.
    Timu hiyo inatarajia kundoka kurejea Monrovia, Aprili 8 mwaka huu kupitia Nairobi, Kenya saa 11.10 alfajiri kwa ndege.
    Azam ilishinda mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza mjini Monrovia wiki mbili zilizopita na sasa inahitaji hata sare katika mchezo wa Jumamosi ili kusonga mbele.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: VIBONDE WA AZAM WAJA KESHO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top