MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uholanzi, Robin van Persie ameihakikishia ubingwa wa 20 wa Ligi Kuu ya England Manchester United usiku huu baada ya kufunga mabao yote katika ushindi wa 3-0 Uwanja wa Old Trafford dhidi ya Aston Villa walio kwenye hatari ya kushuka.
Van Persie alipiga Hat-trick hiyo ndani ya dakika 33 za mechi hiyo, likiwemo bao lililoingia kwenye kinyang'anyiro cha bao bora la msimu alipounganisha moja kwa moja pasi ndefu ya Wayne Rooney akiwa nje kidogo ya eneo la hatari.
Mdachi huyo, aliyeamua kujiunga na kikosi cha Sir Alex Ferguson badala ya Manchester City ya Roberto Mancini msimu huu akitokea Arsenal, alifunga mabao yake katika dakika za pili, 12 na 33, mawili pasi za Rooney na moja pasi ya Ryan Giggs.
Ferguson leo alichezesha viungo watatu katikati, Shinji Kagawa, Michael Carrick na Rooney aliyekuwa akiichezesha timu mbili na kufanya kazi nzuri ya kupendeza, akitoa pasi mbili za mabao kabla ya kumpisha Danny Wellbeck dakika ya 72.
Kikosi cha Man United leo kilikuwa; De Gea, Rafael, Evra, Jones, Evans, Valencia, Giggs, Carrick, Kagawa, Rooney/Welbeck dk72 na Van Persie
Aston Villa; Guzan, Vlaar, Bennett/Clark dk80,Baker, Lowton, N'Zogbia/El Ahmadi dk46,Westwood, Delph, Agbonlahor, Benteke na Weimann
Ahueni: Robin van Persie akiinua mikono yake juu baada ya kuihakikishia ubingwa Manchester United
Bao la msimu: Robin van Persie akifunga bao la pili
Mkono mmoja kwenye taji: Van Persie akishangilia baada ya kukamilisha Hat-trick dakika ya 33
Asante ya pasi ya bao: Van Persie akimuinua Wayne Rooney baada ya kumpa pasi ya bao zuri
Kitu: Van Persie akifunga bao la kwanza
Kwaheri Mancini: Ferguson akinyoosha mkono kwa ishara wa kuwaacha porini Man City katika mbio za ubingwa
Lahitaji marekebisho: Bango hili litatakiwa kubadilishwa kabla ya mechi ijayo Old Trafford
Ni tofauti? Van Persie na United wamekuwa na msimu mzuri
Mchuano: Nathan Baker akimpanda Shinji Kagawa wakati wakigombea mpira
.
Kazi ngumu: Christian Benteke (kulia) akipambana na Patrice Evra
Hakuna shaka: Mashabiki wa United wakiwa na bendera kabla ya mechi na Aston Villa