// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MSUVA NA NURDIN BAKARI WAGOMBEA BAO LA UKOMBOZI YANGA MKWAKWANI JANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MSUVA NA NURDIN BAKARI WAGOMBEA BAO LA UKOMBOZI YANGA MKWAKWANI JANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, April 18, 2013

    MSUVA NA NURDIN BAKARI WAGOMBEA BAO LA UKOMBOZI YANGA MKWAKWANI JANA

    Tazama hapa, Nurdin anatoka kushangilia kama aliyefunga, na Msuva yupo nyavuni na mpira...je, nani kafunga?

    Na Mahmoud Zubeiry, Tanga
    WACHEZAJI wa Yanga, Simon Msuva na Nurdin wameingia katika vita ya kugombea bao la kusawazisha kwa timu yao jana Uwanja wa Mkwakwani, Tanga dhidi ya JKT Mgambo timu hizo zikitoka sare ya 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Ilionekana kama kiungo wa pembeni, Msuva ndiye aliyefunga bao hilo dakika ya 86 na hata alipulizwa na BIN ZUBEIRY baada ya mechi, alisema; “Ni mimi ndiye niliyefunga, Nurdin hakuugusa ule mpira,”.
    Lakini BIN ZUBEIRY alipozungumza na Nurdin baadaye, naye akasema; “Lile bao nimefunga mimi, yeye kapiga mpira kipa wa Mgambo alikuwa anataka kuudaka mimi nikamuwahi kuusukuma nyavuni,”alisema.
    Sare ya jana inamaanisha mbio za ubingwa bado zinaendelea kati ya Yanga SC yenye pointi 53 kileleni sasa na Azam FC yenye pointi 47.
    Hadi mapumziko, Mgambo walikuwa tayari mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na Issa Kanduru aliyemgeuza kwenye eneo la hatari beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kabla ya kumtungua Ally Mustafa ‘Barthez’, baada ya kupokea pasi nzuri ya Salum Mlima.
    Mgambo walitawala sehemu kubwa ya mchezo wa kipindi cha kwanza na kupeleka mashambulizi mengi zaidi langoni mwa Yanga, ambayo zaidi walikuwa wakipiga mirefu kwa lengo la kushambulia moja kwa moja.
    Mchezo pia ulikuwa wa ‘kibabe’ na dakika 45 za kwanza zilimalizika kiungo Frank Domayo akiwa ana ngeu jicho la kushoto baada ya kupigwa kisukusuku na mchezaji mmoja wa Mgambo.
    Dakika 44 zilitosha kwa Hamizi Kiiza katika mchezo wa leo, baada ya kugongwa na beki mmoja wa Mgambo na kushindwa kuendelea na mchezo, akimpisha Said Bahanuzi.
    Kipindi cha pili, Yanga SC ilianza na mabadiliko, ikiwatoa Domayo aliyeumia na nafasi yake kuchukuliwa na Nurdin Bakari na baadaye Oscar Joshua akampisha Haruna Niyonzima.
    Mabadililo hayo yaliongeza uhai katika Yanga SC na kuanza kulishambulia lango la Mgambo JKT mfululizo hatimaye dakika ya 86 wakapata bao la kusawazisha.
    Kutokana na bao hilo kupewa Simon Msuva, sasa anatimiza mabao saba tangu asajiliwe Yanga SC msimu huu katika mechi 28 alizocheza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MSUVA NA NURDIN BAKARI WAGOMBEA BAO LA UKOMBOZI YANGA MKWAKWANI JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top