MANCHESTER United imelazimishwa sare ya 2-2 na wenyeji West Ham United jana katika mchezo wa Ligi Kuu England.
Mabao ya West Ham yalifungwa na Ricardo Vaz Te dakika ya 16 na Mohamed Diame dakika ya 55, wakati ya Man U yalitiwa kimiani na Antonio Valencia dakika ya 31 na Robin van Persie, aliyewanusuru Mashetani Wekundu kupoteza mechi dakika ya 76.
Katika mchezo huo, kikosi cha West Ham United kilikuwa: Jaaskelainen, Demel, Collins, Reid, O'Brien, Diame/Taylor dk82, Nolan/Collison dk82, O'Neil/Noble dk67, Jarvis, Carroll na Vaz Te
Manchester United: De Gea, Da Silva, Ferdinand, Vidic, Evra, Valencia, Carrick, Jones, Kagawa/Hernandez dk77, Rooney/Giggs dk71 na Van Persie.
Shangwe za bao la ukombozi: Robin van Persie aikishangilia bao lake la kusawazisha na Ryan Giggs.
Katika mechi nyingine, Chelsea iliilaza Fulham mabao 3-0, yaliyotiwa kimiani na David Luiz dakika ya 30 na John Terry mawili dakika za 43 na 71.
Kikosi cha Chelsea kwenye mechi hiyo kilikuwa; Cech, Ivanovic, David Luiz, Terry, Bertrand, Ramires/Mikel dk75, Lampard, Mata/Ba dk80, Moses, Hazard/Oscar dk69 na Torres.
Fulham; Schwarzer, Riise (Rodallega, 67),Senderos, Hangeland, Riether, Karagounis/Frimpong dk76, Emanuelson, Enoh, Berbatov, Petric/Frei dk82 na Ruiz.
Tabasamu: Mfungaji wa mabao mawili ya Cheslea, John Terry akishangilia na wenzake
Katika mchezo mwingine, bao pekee la Carlos Tevez dakika ya 83 lilitosha kuwapa mabingwa watetezi, Manchester City ushindi wa 1-0 dhiai ya Wigan. Kikosi cha Man City kilikuwa; Hart, Richards/Sinclair dk83, Kompany, Lescott, Kolarov, Nasri, Garcia/Milner dk59, Barry, Y Toure, Aguero/Dzeko dk46 na Tevez.
Mkombozi: Carlos Tevez akifunga bao pekee na chini akishangilia