KLABU ya Manchester United ya England imeng'olewa kileleni katika orodha ya jarida la Forbes la klabu tajiri duniani na sasa vigogo wa Hispania, Real Madrid ndio wanaongoza.
United imekuwa kileleni tangu wachambuzi wa biashara wa Forbes waanze kuorodhesha klabu tajiri duniani mwaka 2004, lakini sasa imepigwa bao na Real.
Barcelona inashika nafasi ya tatu na Arsenal ni ya nne mbele ya Bayern Munich iliyo katika nafasi ya tano.
Wamepitwa: Manchester United wameporomoka nafasi moja katika orodha ya klabu tajiri kwenye jarida la Forbes
Wako juu: Vigogo wa Hispania, Real Madrid wana thamani ya Pauni Bilioni 2.15
Real ina thamani ya Pauni Bilioni 2.15 (sawa na dola za Kimarekani Bilioni 3.3) - hivyo kuifanya klabu hiyo ya Hispania kuwa chombo cha michezo chenye thamani kubwa zaidi duniani- na United wana thamani ya Pauni Bilioni 2.07.
Wamo nne bora: Arsenal wanashika nafasi ya nne nyuma ya Real Madrid, Manchester United na Barcelona