// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); DROGBA NA ETO'O WATENGEWA TUZO AMBAYO MESSI HATII MGUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE DROGBA NA ETO'O WATENGEWA TUZO AMBAYO MESSI HATII MGUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, April 22, 2013

    DROGBA NA ETO'O WATENGEWA TUZO AMBAYO MESSI HATII MGUU

    Drogba kulia na Eto'o kushoto; Tuzo hii Messi hatii mguu kwa sababu bado kinda

    Na Naseem Mahmoud
    WASHAMBULIAJI bora kuwahi kutokea barani Afrika, Didier Drogba na Samuel Eto’o wameingizwa kwenye orodha ya kuwania tuzo ya Guu la Dhahabu mwaka 2013, kufuata nyayo za mshambuliaji wa Paris Saint Germain ya Ufaransa, Zlatan Ibrahimovic, aliyeshinda mwaka jana.
    Manahodha hao wa Ivory Coast na Cameroon ni Waafrika pekee katika orodha ya wachezaji tisa walioingizwa kwenye kinyang’anyiro cha tuzi hiyo, inayotolewa kwa wachezaji wenye mafanikio makubwa na mwonekano mzuri.
    Wawania tuzo hiyo wengine ni Mfaransa David Trezeguet, Mjerumani Miroslav Klose, Mtaliano Andrea Pirlo, Waspanyola Andres Iniesta na Iker Casillas na Waingereza Franck Lampard na David Beckham.
    Tuzo huyo Guu la Dhahabu inatolewa kwa mchezaji aliye uwanjani ambaye angalau ana umri usiopungua miaka 29 na hawezi kushinda zaidi ya mara moja
    Washindi wa awali wa tuzo hiyo ni; 2003: Roberto Baggio (Italia, Brescia) 2004: Pavel Nedved (Jamhuri ya Czech, Juventus) 2005: Andryi Shevchenko (Ukraine, AC Milan) 2006: Ronaldo (Brazil, Real Madrid) 2007: Alessandro Del Piero (Italia, Juventus) 2008: Roberto Carlos da Silva (Brazil, Fenerbahçe) 2009: Ronaldinho (Brazil, AC Milan) 2010: Francesco Totti (Italia, Roma) 2011: Ryan Giggs (Wales, Manchester United) na 2012: Zlatan Ibrahimovic (Sweden, Paris SG).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: DROGBA NA ETO'O WATENGEWA TUZO AMBAYO MESSI HATII MGUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top