Bao dakika ya mwisho: David Luiz akifunga kwa mpira wa adhabu kuipa ushindi wa 2-1 Chelsea ugenini usiku huu
Shangwe zake: Luiz akishangilia baada ya kufunga
Penalti ya utata: Fabian Schar akiifungia Basle kwa penalti bao la kusawazisha
BAO la dakika ya mwisho la mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja nyavuni la David Luiz limeipa ushindi wa mabao 2-1 Chelsea katika Nusu Fainali ya kwanza ya Europa League ugenini dhidi ya wenyeji Basle.
Awali, alinusurika kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kudaiwa kucheza rafu.
Refa Pavel Kralovec alitoa uamuzi wa ajabu sana alipodai Luiz kamchezea rafu Cesar Azpilicueta kwenye eneo wakati hakucheza na akawapa penalti wenyeji wakapata bao la kusawazisha lililofungwa na Fabian Schar dakika ya 87.
Chelsea ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Victor Moses dakika ya 12.
Kikosi cha Basle kilikuwa: Sommer, Philipp Degen, Schar, Dragovic, Park, Fabian Frei, Salah/Degan dk78, El-Nenny/Zoua dk65, Die/Diaz dk61, Stocker na Streller.
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Terry, Cole, Luiz, Hazard/Mata dk71, Ramires, Lampard/Oscar dk79, Moses na Torres.
Katika Nusu Fainali nyingine, Fenerbace imeilaza 1-0 nyumbani Benfica, bao pekee la Korkmaz dakika ya 72.
Katika Nusu Fainali nyingine, Fenerbace imeilaza 1-0 nyumbani Benfica, bao pekee la Korkmaz dakika ya 72.
Bao la kwanza: Victor Moses (kulia) akiifungia Chelsea
Sarakasi za shangwe: Winga Mnigeria akishangilia kwa sarakasi za aina yake
Malengo makubwa: Rafa Benitez anataka kuipa Chelsea taji la Europa League msimu huu
Mchawi: Hadi anatolewa, Eden Hazard alikuwa nyota wa mchezo