MABAO mawili ya mikwaju ya penalti kipindi cha pili yaliyofungwa na Graham Burke yameiwezesha Aston Villa kutwaa ubingwa wa vijana Ulaya katika michuano ya NextGen Series.
Nyota hao makinda wamekumbushia mafanikio ya timu ya wakubwa, iliyoshinda taji hilo a Ulaya mwaka 1982.
Katika mchezo huo, kikosi cha Chelsea kilimkosa Mtanzania Adam Nditi, kilikuwa; Beeney, Christiensen, Davey/Colkett, Pappoe, Wright, Ake, Kiwomya, Loftus-Cheek/Hunte, Feruz, Baker na Boga
Aston Villa: Watkins, Webb, Kinsella, Calder, Donacien, Lewis, Barton, Carruthers, Robinson, Burke na Grealish
Wakati wa kusherehekea: Aston Villa wakishangilia baada ya kuichapa Chelsea katika fainali ya NextGen Series jana
Mpambano: Graham Burke (kushoto) wa Aston Villa akimtoka Danny Pappoe wa Chelsea