KLABU ya Arsenal imepiga hatua katika mbio zake za kuwania saini ya Stevan Jovetic baada ya kuanza mazungumzo na klabu yake, Fiorentina.
Habari zinasema kwamba, kocha Arsene Wenger anaihofia Chelsea kwa namna ilivyopanga kujisuka upya.
The Gunners wamekuwa wakimfuatilia Jovetic, mwenye umri wa miaka 23, tangu mwaka 2011 na wakati klabu hiyo ya Serie A inamthaminisha kwa kiasi cha Pauni Milioni 25, Arsenal — ambayo ina bajeti ya Pauni Milioni 70 za usajili, inataka ipunguziwe bei ya kumnunua mchezaji huyo
Anatakiwa sana: Arsenal iko tayari kumwaga mpunga kwa ajili ya Stevan Jovetic
Hatua ya klabu hiyo kufanya jitihada za mapema kumnasa Jovetic ni dalili nzuri, haswa ikizingatiwa Manchester City na Juventus zote zinamtaka mshambuliaji huyo. Dili lolote litategemea na Arsenal kama itafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Wenger, pia anatazamia kumsajili kipa mpya wa kwanza, na amekuwa akimmulika mlinda mlango wa Hamburg, Rene Adler tangu Machi.
BIN ZUBEIRY inatambua msaka vipaji mkuu wa Arsenal, atatoa uamuzi wa mwisho juu ya kipa huyo mwenye umri wa miaka 28, baada ya mechi ya Jumapili dhidi ya Schalke. Arsenal inaona kulikoni kutoa Pauni Milioni 15 kuwanunua ama kipa wa Stoke, Asmir Begovic au wa Sunderland, Simon Mignolet, bora kutoa Pauni Milioni 8 kumnasa kipa huyo Mjerumani.
Wenger anataka kuboresha kikosi chake kujiandaa kupambana na Chelsea ambayo iko mbioni kuwasajili kiungo mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Andre Schurrle na mshambuliaji wa Atletico Madrid, Radamel Falaco.
Mikono salama: Arsenal pia inamtaka kipa wa Hamburg, Rene Adler
Woga: Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anaihofia Chelsea ilivyopanga kumwaga mpunga kusajili
Wenger amesema: "NInahofia na kitu wanachoweza kufanya Chelsea mwishoni mwa msimu. Tunatakiwa kujiandaa kwa ajili yao kwa kuwa moja ya klabu zilizowekeza.".
Wakati huo huo, Alex Oxlade-Chamberlain amesema amechoka maisha ya benchi.
Winga huyo amecheza mechi 11 tu katika kikosi cha kwanza Arsenal kwenye Ligi Kuu msimu huu.
Wawili matatizo: Chelsea inatumai kumsajili Andre Schurrle (juu) na Radamel Falaco (chini)