KLABU ya Bayern Munich wameanza vyema kampeni ya kuelekea kucheza fainali ya tatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ndani ya miaka minne, baada ya kuikung'uta Barcelona mabao 4-0 usiku huu kwenye Uwanja wa Allianz Arena katika Nusu Fainali ya kwanza.
Mabao mawili kutoka kwa Thomas Muller na moja kwa kila mmoja, Mario Gomez na Arjen Robben yamempa faraja kocha Jupp Heynckes ambaye sasa sijui itokee miujiza gani Jumatano ijayo Uwanja Nou Camp kwenye mchezo wa marudiano akose tiketi ya kwenda Wembley.
Kikosi cha Bayern Munich kilichofanya mauaji hayo kilikuwa: Neuer, Lahm, Boateng, Dante, Alaba, Javi Martinez, Schweinsteiger, Robben, Muller/Pizarro dk83, Ribery/Shaqiri dk88 na Gomez/Gustavo dk71.
Barcelona: Valdes, Dani Alves, Pique, Bartra, Jordi Alba, Xavi, Busquets, Iniesta, Sanchez, Messi na Pedro/Villa dk83.
Mbele kwa mbele: Thomas Mueller akishangilia baada ya kuifungia Bayern bao la kwanza
Mguu mmoja fainali: Nyota wa Bayern Munich, Mario Gomez na mchezaji mwenzake, Javi Martinez wakishangilia baada ya kupata bao la pili
La tatu kiulainiiii: Arjen Robben akishangilia baada ya kufunga bao la tatu dhidi ya Barca
kumbuka jina: Robben akishangilia mbele ya mashabiki baada ya kufunga bao lake
Wapoleee: Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi akionekana aliyekata tamaa
Hakuna kurudi nyuma? Messi na Barcelona wanakabiliwa na mchezo mgumu wa marudiano