// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); 'YANGA ONE' BARTHEZ MGONJWA, HATARINI KUKOSA MECHI YA JUMAMOSI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE 'YANGA ONE' BARTHEZ MGONJWA, HATARINI KUKOSA MECHI YA JUMAMOSI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, March 07, 2013

    'YANGA ONE' BARTHEZ MGONJWA, HATARINI KUKOSA MECHI YA JUMAMOSI

    Barthez amedaka kwa umahiri na maarifa mechi zilizopita za Ligi Kuu kiasi cha kuiweka Yanga kileleni

    Na Mahmoud Zubeiry
    KIPA namba moja wa Yanga, Ally Mustafa Mtinge ‘Barthez’ yuko kwenye hatihati ya kusimama langoni keshokutwa timu yake ikimenyana na Toto Africans ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya tumbo.
    Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto ameiambia BIN ZUBEIRY mchana wa leo kwamba, Barthez ameshindwa kufanya mazoezi na wenzake leo kutokana na kusumbuliwa na tumbo.
    “Lakini hatutarajii kama itakuwa ni kitu cha muda mrefu, tunasikilizia afya yake bado, tuna matumaini atakuwa fiti na kucheza Jumamosi,”alisema Kizuguto.
    Aidha, Kizuguto alisema beki Juma Abdul pia naye leo hajafanya mazoezi kutokana na kusumbuliwa na homa.
    Kizuguto alisema majeruhi ambaye anawaumiza kichwa kwa sasa ni Nurdin Hamadi Bakari ambaye anasumbuliwa na maumivu ya goti. Alisema kiungo huyo rasta anaweza kufanyiwa upasuaji wiki ijayo baada ya kufanyiwa vipimo jana.
    Kuhusu beki Ladislaus Mbogo ambaye wanataka kumfanyia upasuaji wa uvimbe kwenye shavu lake, Kizuguto alisema naye pia atafanyiwa zoezi hilo wiki ijayo.
    Kizuguto amesema kikosi kizima cha Yanga kimeingia kambini leo, katika hosteli za klabu hiyo, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya Toto.
    Yanga inaongoza Ligi Kuu kwa sasa kwa pointi zake 42, baada ya kucheza mechi 18, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 36, baada ya kucheza mechi 18 pia, wakati mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 31 sawa na Coastal Union ya Tanga na Mtibwa Sugar ya Morogoro wanashika nafasi ya tatu, wakibebwa na wastani wao mzuri wa mabao.

                           P W D L GF GA GD Pts
    1 Yanga 18 13 3 2 35 12 23 42
    2 Azam 18 11 3 4 31 15 16 36
    3 Simba SC 18 8 7 3 26 15 11 31
    4 Coastal U 19 8 7 4 21 16 5 31
    5 Mtibwa 20 8 7 5 22 18 4 31
    6 Ruvu Shooting 18 8 5 5 21 17 4 29
    7 Kagera Sugar 19 7 7 5 19 17 2 28
    8 JKT Oljoro 19 6 6 7 20 22 -2 24
    9 Mgambo JKT 20 7 3 10 14 19 -5 24
    10 TZ Prisons 20 4 8 8 11 17 -6 20
    11 JKT Ruvu 18 5 4 9 16 28 -12 19
    12 Polisi Moro 18 3 6 9 9 18 -9 15
    13 Toto African 19 2 8 9 15 27 -12 14
    14 African Lyon 20 3 4 13 13 32 -19 13
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: 'YANGA ONE' BARTHEZ MGONJWA, HATARINI KUKOSA MECHI YA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top