FIFA itaamua kumuadhibu au la Luis Suarez mara itakapopata ripoti ya refa aliyechezesha mechi kati ya Uruguay na Chile kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
Mshambuliaji huyo wa Liverpool alinaswa na kamera za Televsheni akimrupia konde mchezaji wa Chile, Gonzalo Jara, lakini Nestor Pitana, Ofisa wa mechi hakulinukuu tukio hilo, baada ya kuzungumza na wawili hao kufuatia kuvurugana kwao wakati wa kona.
Ikiwa itabainika ni kweli alifanya hivyo, Suarez atakuwana na rungu la FIFA ingawa haiwezi kufanya hivyo hadi ipate ripoti rasmi ya refa ya maandishi.
Tukio: Luis Suarez akimchapa konde Gonzalo Jara usoni.
Kifungoni: Suarez tayari atatumikia adhabu ya kadi za njano.
Msemaji wa FIFA amesema: "Tutaendelea kukusanya ripoti zote za mechi, kwa kuwa marefa wana saa 24 ya kuwasilisha ripoti hizo. Tutaangalia kilichomo kwenye ripoti zao, kisha FIFA itachukua hatua kwa mujibu wa ripoti hizo."
Suarez tayari anakabiliwa na adhabu ya kusimamishwa baada ya kupewa kadi ya njano dakika za lala salama katika medhi dhidi ya Chile kwa utovu wa nidhamu.
Atakosa mechi ijayo ya Urugay dhidi ya Venezuela mwezi Juni kuwania Fainali za Brazil, ambayo ni habari njema kwa klabu yake Liverpool.