• HABARI MPYA

        Monday, March 18, 2013

        SANGA, DK KATUNDU, MADEGA WAONGOZA MAZISHI YA ZOLA WA YANGA JIONI YA LEO KISUTU



        Mwili wa marehemu Hamza Said 'Zola' (katika picha ndogo) ukiwasili makao makuu ya klabu kwa ajili ya kuangwa na wapenzi wa soka, washabiki na wanachama kabla ya kupelekwa katika makaburi ya Kisuru kwa mazishi leo.

        Na Mwandishi Wetu
        MAMIA ya wanachama, wapenzi na mashabiki wa soka leo jioni wameshiriki katika safari ya mwisho ya kuusindikiza mwili wa aliyekuwa mfanyakazi wa klabu ya Yanga, marehemu Hamza Said ‘Zola’, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jana mjini Dar es Salaam, ambaye amezikwa katika makaburi ya Kisutu, Dar es salaam.
        Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga akiweka
         mchanga katika kaburi la marehemu Hamza Zola

        Mazishi ya Zola yaliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, Wenyekiti wa zamani wa klabu, Mzee Dk. Jabir Idrisa Katundu, na Wakili Iman Omar Madega na viongozi wengine mbalimbali waliowahi kuongoza klabu hiyo ya kihistoria nchini.
        Marehemu Zola ambaye alifikwa na umauti jana alfajiri katika makutano ya mitaa ya Rufiji na Kongo kwa ajali ya kugongwa na gari, alikua akitokea mitaa ya Kariakoo akitembea kuelekea makao makuu ya klabu na ndipo gari hilo lilipomgonga kwa nyuma wakati akitembea kuelekea klabuni.
        Uongozi unatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki na wapenzi wa soka nchini kwa kuondokewa na rafiki yetu kipenzi.  
        Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments
        Item Reviewed: SANGA, DK KATUNDU, MADEGA WAONGOZA MAZISHI YA ZOLA WA YANGA JIONI YA LEO KISUTU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry