KLABU ya Paris Saint-Germain inajipanga kukata dau nono ili kumsajili Samir Nasri, ambaye mambo hayamuendei vizuri kwa sasa Manchester City.
Vyanzo kutoka Manchester City vimesema kwamba mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa yuko tayari kuondoka Uwanja wa Etihad, baada ya kupoteza uhusiano mzuri na kocha Roberto Mancini.
Nasri inaelezwa amekasirishwa na kukerwa kitendo cha kocha wake kumkandia hadharani wiki iliyopita.
Samir Nasri anaweza kuondoka Manchester City kuhamia PSG