MSHAMBULIAJI Wayne Rooney anakabiliwa na kibarua kigumu cha kunusuru nafasi yake katika kikosi cha Manchester United baada ya kocha Sir Alex Ferguson kuendelea kutilia shaka uimara na uwezo wake kwa ujumla.
Ferguson alifanya kitu cha ajabu, akimuanzishia benchi mshambuliaji huyo wa England katika mechi ya juzi usiku ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid Uwanja wa Old Trafford.
Kocha wa United anaamini Rooney ameshindwa kupambana na uzito na majeruhi, mambo ambayo yananyonya soka yake.
Wayne Rooney akitokea benchi juzi
Uhusiano wa Rooney na kocha wake sasa unatia shaka Old Trafford
Rooney, mwenye umri wa miaka 27, akiwa anaingia katika miaka miwili ya mwisho ya mkataba wake mwishoni mwa msimu huu, Ferguson anafahamu ana uamuzi wa kuchukua juu ya mustakabali wake.
Kwa jinsi ilivyo, Mscotland huyo hatakataa kumuuza iwapo klabu itapewa ofa ya zaidi ya Pauni Milioni 20.