NYOTA Cristiano Ronaldo amerejea Manchester na kuifungia bao la ushindi Real Madrid lililoitoa timu yake ya zamani katika Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Old Trafford.
Sir Alex Ferguson alimuanzishia benchi Wayne Rooney, lakini wenyeji ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao mapema kipindi cha pili, baada ya Sergio Ramos kujifunga.
Lakini mambo yaliwaharibikia baadaye kidogo tu Man United, baada ya Luis Nani kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumchezea rafu Alvaro Arbeloa.
Na baada ya hapo, bao la Luka Modric lilifuatiwa na bao la Ronaldo dakika tatu baadaye, hivyo vigogo hao wa Hispania kutinga Robo Fainali.
VIKOSI, WAFUNGAJI...
Man United: De Gea, Da Silva (Valencia 87), Vidic, Ferdinand, Evra, Carrick, Cleverley (Rooney 73), Nani, Welbeck (Young 80), Giggs, van Persie.
Benchi: Lindegaard, Evans, Hernandez, Kagawa.
Kadi za njano: Evra, Carrick
Kadi nyekundu: Nani dk57.
Mfungaji: Ramos (Kujifunga) dk48.
Real Madrid: Diego Lopez, Arbeloa (Modric 59), Varane, Sergio Ramos, Fabio Coentrao, Khedira, Alonso, Di Maria (Kaka 42), Ozil (Pepe 71), Ronaldo,Higuain.
Benchi: Adan, Benzema, Albiol, Callejon.
Kadi za Njano: Arbeloa, Pepe
Wafungaji: Modric dk67, Ronaldo dk69.
Refa: Cuneyt Cakir (Uturuki)
Mahudhurio: 74,959
Mshindi wa mechi: Bao la Ronaldo limeitoa timu yake ya zamani
Kiungo wa zamani wa Spurs, Modric akifunga bao la kusawazisha
Nje; Ronaldo akifunga bao lililoitupa nje United
Beki wa Real akijifunga
Kadi nyekundu: Hapa ndipo ilipofia United baada ya kupungukiwa mchezaji mmoja
Akitokea benchi: Rooney akipasha kutokea benchi
Welbeck alikaribia kufunga leo, lakini alikuwa ameotea
Vidic alipiga kichwa kikagonga mwamba kipindi cha kwanza
Giggs amecheza mechi ya 1,000 leo Man United
Ronaldo amepata mapokezi mazuri leo Old Trafford
Ronaldo alikuwa katika wakati mzuri leoOld Trafford
Ronaldo akipasua Old Trafford
Ronaldo alicheza kwa raha leo