// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RONALDO AREJEA MANCHESTER, GIGGS MECHI YA 1,000 KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RONALDO AREJEA MANCHESTER, GIGGS MECHI YA 1,000 KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Monday, March 04, 2013

        RONALDO AREJEA MANCHESTER, GIGGS MECHI YA 1,000 KESHO


        NYOTA Cristiano Ronaldo na Galacticos wa Real Madrid wametua katika ardhi ya Manchester jana usiku tayari kwa mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya wenyeji Manchester United.
        Nyota huyo wa zamani wa United, ambaye atacheza kwenye Uwanja wa Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu auzwe kwa Pauni Milioni 80 zilizoweka rekodi ya dunia kwenda Madrid mwaka 2009, alipokewa vema na mashabiki wa Jiji hilo katika Uwanja wa ndege wa Manchester.
        Lakini Mreno huyo lazima amesahau kuhusu baridi kali la mji wa Manchester mwezi Machi, kwani alipofika katika Lounge akiwa amevaa jezi na bukta na kujikuta akipandisha soksi zake kutokana na baridi hilo.
        He's back: Cristiano Ronaldo touches down in Manchester ahead of the crucial second-leg Champions League tie on Tuesday
        Amerejea: Cristiano Ronaldo ametua katika ardhi ya Manchester kwa ajili ya mechi ya kesho na Man United
        But what is he wearing: Manchester in March is a bit cold for shorts, Cristiano
        Amevaaje? Jiji la Manchester linakuwa na baridi kali mwezi Machi, haliendani na mavazi haya ya Ronaldo

        Mechi ya kesho imekaa vizuri kwa United ambao walianza kwa sare ya 1-1 ugenini Uwanja wa Bernabeu wiki tatu zilizopita.
        Ronaldo alisawazisha bao baada ya Danny Welbeck kutangulia kufunga kipindi cha kwanza, lakini Sir Alex Ferguson atakuwa mwenye kujiamini akivaana na Jose Mourinho.
        Madrid nao wa ko vizuri, wakitoka kushinda mechi mbili mfululizo ngumu ndani ya siku tano dhidi ya mahasimu wao, Barcelona, ya kwanza ya Kombe la Mfalme na nyingine ya Ligi Jumamosi.
        United nao wako sawa, wakiwa wanaongoza Ligi Kuu England kwa wastani wa pointi 15 zaidi dhidi ya jirani zao Manchester City.
        In the balance: Ronaldo's brilliant header has left this tie closer teetering on a knife-edge
        Bao la kusawazisha: Ronaldo akifunga kwa kichwa maridadi bao la kusawazisha dhidi ya United mechi ya kwanza
        Waiting patiently: A mob of people await the arrival of Ronaldo and his Real Madrid team-mates at Manchester airport on Sunday night
        Wanamsubiri mfalme: Kundi la mashabiki likimsubiri Ronaldo na Real Madrid yake wawasili Uwanja wa Ndege wa Manchester jana usiku
        Old foe: Real Madrid manager Jose Mourinho (above) will prepare to lock horns with Sir Alex Ferguson (below) once more
        Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho akiwasili
        Sir Alex Ferguson
        Ronaldo atapewa mapokezi mazuri Old Trafford, lakini haifahamiki atafanya nini kama ataweza kufunga bao dhidi ya timu yake ya zamani.
        "Nina uhakika mashabiki wa United watanipokea vizuri, kama nitafunga dhidi yao, itakuwa baaba kubwa,"alisema.
        "Siwezi kusema nitafanya nini. litakuwa jambo moja la kufurahisha, lakini ningependa kuwa katika mazingira hayo,"alisema Ronaldo.
        Up close and personal: One fan tries to get a little bit too close to the £80 million man
        Up close and personal: One fan tries to get a little bit too close to the £80 million man
        Memories: A fan holds up a Ronaldo shirt from his days at United. The Portuguese is unsure what he will do should he score against his former team
        Kumbukumbu: Shabiki akiwa amevaa jezi ya Ronaldo enzi zake akiwa United.
        Looking good: Real Madrid will train at Manchester City's Carrington training ground
        Real Madrid atafanya mazoezi katika Uwanja wa Manchester City, Carrington

        Ronaldo amebakiza miaka miwili katika mkataba wake Real na mazungumzo kwa ajili ya mkataba mpya yanaendelea. 
        Wakati huo huo, Ryan Giggs anatarajiwa kucheza mechi ya 1,000 kesho wakati miamba hiyo ikiumana.
        1,000 not out: Ryan Giggs is expected to make his 1,000th senior appearance in the match
        Mechi ya 1,000: Ryan Giggs anatarajiwa kucheza mechi ya 1,000 kesho
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments
        Item Reviewed: RONALDO AREJEA MANCHESTER, GIGGS MECHI YA 1,000 KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry