• HABARI MPYA

        Thursday, March 21, 2013

        RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA MRADI WA UJENZI WA UWANJA WA KISASA WA AZAM LEO

        Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Azam, Sheikh Said Mohamed kabla ya kuzindua jiwe la Msingi wa ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa Azam FC mchana wa leo, makao makuu ya klabu hiyo, Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

        Rais Kikwete akikata utepe tayari kuzindua mradi wa ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa Azam FC. Wengine kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meckysadik, Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya S.S. Bakhresa, wamiliki wa Azam FC, Abubakar Said Salim Bakhresa na kushoto ni Sheikh Said na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara.

        JK akipenua pazia kufungua jiwe la Msingi

        Msafara; Rais JK akiwapungia mkono wananchi wakati wa kuzindua mradi huo

        Rais JK na msafara wake akipita pembezoni mwa bwawa la kuoghelea la Azam Complex

        Rais JK akipata maelekezo kutoka kwa Daktari wa Azam FC, Mjerumani Paulo Gomez ndani ya Gym ya kisasa ya iliyopo ndani ya Azam Complex

        Sheikh Said akimuelekeza jambo Rais JK wakati akimtembeza katika himaya ya Azam Complex

        • Blogger Comments
        • Facebook Comments
        Item Reviewed: RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA MRADI WA UJENZI WA UWANJA WA KISASA WA AZAM LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry