Wayne Rooney alikuwa mchezaji wa kwanza kuanza mazoezi kwenye kikosi cha Roy Hodgson, mwanzo wa wiki, akitaniana na Leon Osman, akichezea mpira kwenye uwanja wa Staffordshire.
Hii hamu yake ya kitoto ya kupenda kucheza mpira bado anayo.
“Kipaji cha Rooney kilitengenezwa kwenye mitaa ya Croxteth,” alisema Steven Gerrard. “akitoka tu nje ya nyumbani kwa alikuwa akiingia uwanjani, bila onyo, wala hofu.”
Hasomeki: Wayne Rooney hajawahi kufanya makubwa akiwa na England kama wengi walivyomtabiria
Gerrard aliandika haya kwenye kitabu cha maisha yake akihusisha na mechi ya kwanza ya Rooney akiw ana timu ya taifa dhidi ya Uturuki, miaka 10 iliyopita.
England walishinda 2-0 mabao ya Darius Vassell na David Beckham, lakini alikuwa ni kijana mdogo ambaye Sven Goran Eriksson alimpanga kwa mara ya kwanza aliyewaacha midomo wazi watu walioshuhudia pambano hilo pale Stadium of Light, wengi walikiri kijana huyo alikuwa wa kipekee.
Gary Lineker alisema kuwa kijana huyo alimuacha mdomo wazi. Eriksson alisema: “Sioni sababu ya kumuweka benchi kama anacheza hivi”
Toka wakati huo hakuna kocha wa England aliyemuweka benchi. Labda awe na majeruhi, amefungiwa au kumpumzisha ili kumfurahisha Sir Alex Ferguson. Mpaka sasa anamechi 79 za timu ya taifa.
Mzoefu: Rooney alicheza mechi yake ya kwanza England akiwa kinda
Kadi nyekundu ya kwanza: Rooney alipewa kadi nyekundu ya kwanza wakati wa robo fainali ya Kombe la Dunia 2006, dhidi ya Ureno
Kuropoka: Rooney amekuwa akipondwa na mashabiki wa England kutokana na kufanya vibaya kwa timu hiyo
Kikosi cha Hodgson, kinaenda kupambana na San Marino huku Rooney akiwa haeleweki. Anaonekana kama ameelemewa na mzigo wa kuwa mchezaji bora wa England na uzito wa mataraji anayowekewa na watu tangu alipofanya vizuri kwenye michuano ya Euro 2004.
Siku ambayo Rooney alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na timu ya taifa dhidi ya Uturuki, pacha wake alikuwa Michael Owen, ambaye ametangaza kutundika daluga mwisho wa msimu huu.
Uti wa Mgongo: Pacha wa zamani wa Rooney, Michael Owen alikuwa balaa timu ya taifa
Uamuzi wa Owen kutundika daluga umepokewa jwa hisia tofauti, alifunga mabao 40 akiwa na timu ya taifa, ikiwa ni pamoja na bao zuri dhidi ya Argentina, hat-trick dhidi ya Ujerumani, bao dhidi ya Brazil robo fainali ya Kombe la Dunia.
Yako wapi matukio muhimu ya Rooney, ambaye ndiye mfungaji mdogo zaidi wa England, mabao mawili dhidi ya Bulgaria na shuti kali dhidi ya Urusi hayakuwa muhimu sana.
Kadi nyekundu namba 2: Rooney alipewa kadi nyekundu dhidi ya Montenegro
Bao la ushindi la kichwa: Rooney alirudi kwenye timu baada ya adhabu na kufunga dhidi ya Ukraine
Kiboko ya Samba? Rooney pia alifunga kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Brazil
Kichwa cha karibu dhidi ya Ukraine, jijini Donetsk kilikuwa muhimu kwa England kusonga mbele wakati wa michuano ya Euro 2012, lakini lilikuwa bao lake la kwanza kwenye mechi ya kimataifa baada ya miaka nane.
Cha kusikitisha ni kwamba kadi nyekundu dhidi ya Ureno na Montenegro inakaa zaidi kichwani.
Analingana na Owen, kipaji cha kweli kingine. Rooney anamabao saba pungufu ya Owen na mechi 10 pungufu pia, wastania ambao unampa moyo kuelekea mechi ya San Marino, ambayo ndio timu mbovu zaidi duniani.
Zaidi ya haya, mchango wa Rooney hauwezi kuhasabiwa kwa mabao tu. Amecheza pekee mbele, amecheza pacha, kucheza chini kama kiungo mchezeshaji na mara kadhaa pembeni.
Kujitoa kwake uwanjani, muda wote anajituma kutokana na majukumu aliyopewa. Bado yuko hivyo hata akiwa Manchester United. Alicheza mechi dhidi ya Real Madrid ugenini, lakini mechi ya nyumbani alipumzishwa. Je, huu ushahidi kwamba anahama kutoka kuwa mchezeshaji mpaka kuwa mtu wa kujituma uwanjani?
Farasi ka kazi? Je, vipaji vya Rooney havitumiwi ipasavyo?
Bonge la Nyota: Rooney alikuwa balaa Euro 2004
Shujaa mpya: kuibuka kwa Rooney
Mechi ya kwanza: Rooney akicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa
Wakati wa kushereheka: Rooney amekuwa na namba ya kudumu England tangu alipocheza dhidi ya Uturuki
Fabio Capello anaweza kuwa kocha pekee ambaye alikaribia kufichua siri ya Rooney, England. Rooney alifunga nusu ya mabao yake ya mechi za mashindano 24 chini ya Capello. Tisa kati ya hayo kwenye mechi tisa za kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2010, akicheza mbele na Emile Heskey.
Lakini alienda Afrika Kusini kukiwa na hofu juu ya uzima wake, lakini baadaye iliibuka kwamba alikuwa na matatizo ya kifamilia zaidi.
Alikuwa akilinganishwa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, alijawa na hasira kwenye michuano hiyo, akigombana na mshika kibendera wa kike kwenye mechi za kirafiki, alikuwa na majanga kibao kabla ya mechi hizo, mashabiki wa England waliizomea timu baada ya sare ya bila kufunga dhidi ya Algeria.
Baada ya michuano hiyo Rooney alicheza mwaka mzima bila bao, huku pacha wake kwenye safu ya ushambuliaji wakija na kuondoka: Bobby Zamora, Peter Crouch, Darren Bent, Kevin Davies, Ashley Young, Andy Carroll na Danny Welbeck wote hawa wamecheza sambamba an Rooney tangu Kombe la Dunia 2010 lilipomalizika.
Atakosekana: England itamkosa Jack Wilshere
Wakati Hodgson alipochukua mikoba ya kuinoa timu hiyo mwaka jana aliweka wazi kabisa kwamba Rooney ni mchezaji anayewez kucheza nafasi nyingi lakini ni bora zaidi akicheza kama namba 10, au mshambuliaji wa pili.
Mwezi uliopita, kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Brazil, Rooney alikuwa mbele kwenye mfumo wa 4-3-3 ambao uliwekwa ili kumpa nafasi Jack Wilshere. Utafiti huo ulifanya kazi walishinda 2-1 na ushindi huo kwa kiasi kikubwa ulichangiwa na uchezaji wa Wilshere, Rooney na Tom Cleverley.
Je, Hodgson ataendelea kutumia mfumo huu wakati huu ambao Wilshere ni majeruhi au atarudi kwenye mfumo wake wa awali? Kwenye mechi mbili za kufuzu ambazo wamecheza na Rooney akiwepo alicheza sambamba na Welbeck dhidi ya San Marino na Defoe dhidi ya Poland.
Kubadilisha badilisha hakumsaidii Rooney kujitambulisha vizuri kwenye timu ya England.
Gerrard anaweza kumuone huruma kwa sababu imewahi kumkuta, na anaweza kumzungumzia kipekee mchezaji ambaye alikuwa balaa kwenye mechi yake ya kwanza akiwa na miaka 17 lakini ameshindwa kufikia kwenye levo za Messi na Ronaldo.
Akiwa na miaka 27, Rooney anaweza kuwacha alama kwenye soka la kimataifa kwa kufunga mabao ya maana kwenye mechi zijazo na anaweza kuanza hilo kwa kufunga kwenye mechi dhidi ya San Marino kesho na mechi dhidi ya Montenegro, Jumanne.